|
Waandishi wakubali kubadilika, wajifunze Kiswahili
wasirudie makosa
|
|
|
|
|
Na Cosmas Pahalah
KATIKA makala yafuatayo nimetoa maelezo ambayo yana lengo la kusisitiza
baadhi ya mambo yaliyoelezwa hapo awali.
Lengo ni kuimarisha uelewa wa misingi ya lugha sanifu ya Kiswahili. Kwa
mfano:
“ Misitu ya Kazimzimbwi na Pugu iko katika hatari ya kuvamiwa na wananchi kwa
ajili ya kuvuna miti ya kuchomea mkaa.”
Katika sentensi hii msomaji ataelewa kuwa iko miti ya kuchomea mkaa kwa maana
ya kuwa miti ni kichocheo cha kuchoma mkaa. Ukweli ni kuwa miti inachomwa na
matokeo yake ni upatikanaji wa mkaa. Kwa hiyo, sahihi ni kuandika, “…kwa
ajili ya kuvuna miti ya kuchoma mkaa.”
“Kwa bahati nzuri, nilipata fursa ya kuhudhuria mikutano ya kampeni na moja
ya mikutano niliyohudhuria ndiyo msingi wa makala hii.”
Ni kawaida kwa maneno yanayoanza na ‘ma’ kama vile mahitaji, madhumuni,
maradhi na kadhalika, neno linalofuata kama
ni kutoa maelezo ni ‘haya’ kwa mfano, maelezo haya, mahitaji haya, madhumuni
haya, maradhi haya n.k. Vivyo hivyo, tunavyoeleza juu ya makala.
Tunasema makala haya na wala siyo makala hii.
Nafahamu kuwa watu wengi wamezoea kuandika makala hii, lakini mazoea yasiwe
kisingizio cha kuendeleza makosa.
Ni vigumu kubadilika baada ya kuzoea aina fulani ya mazoea, hivyo hatuna budi
kubadilika.
“ Lugha zilizokuwa zikitumiwa na baadhi yao zilikuwa za kejeli dhidi ya viongozi wa
juu wa Chadema.”
Wakati mwandishi alipoandika taarifa hii alisema kuwa wazungumzaji walitumia
lugha za kejeli. Ukweli ni kuwa lugha iliyotumika ni ya Kiswahili na wala
siyo zaidi. Katika lugha hii, wazungumzaji walitumia maneno ya matamshi ya
kejeli na matusi ambayo yalikuwa ni ya udhalilishaji.
Hivyo, ingekuwa bora kama angeandika kuwa
wazungumzaji walitumia maneno au matamshi ya kashfa na wala siyo lugha
za kashfa.
“ Kitu kilichomfanya awe na wakati mgumu ni kwa mpira ilikuwa wa kasi
na wenye rafu nyingi.”
Hapa siyo kitu kimoja kichomfanya awe na wakati mgumu bali ni mambo mengi
yakiwamo kasi ya mpira na pia rafu nyingi.
Liko neno lililotumika la ‘ilikuwa’ lililotumika kimakosa. Ilitakiwa liwe
‘kuwa’. Kwa hiyo, angeandika,
“Kitu kilichomfanya awe na wakati ngumu ni kwa mpira kuwa wa kasi na wenye
rafu.”
“ Hoteli ya Gate Way
jana ilinusurika kuvamiwa na vijana wa Chadema kufuatia madai
kuwa na masanduku ya kura yaliingia katika ngome ya CCM.”
Kwa bahati mbaya mwandishi ana taaluma ndogo ya sarufi kwani ameshindwa
kutambua matumizi sahihi ya ‘o’ rejeshi.
Badala ya kuandika ‘masanduku ya kura yaliingia katika ngome ya CCM’
alitakiwa kuandika masanduku ya kura yaliyoingia katika ngome ya CCM.
“Kwa mfano, ukichukua takwimu za wanafunzi kutoka wilayani ukilinganisha na
zilizoko mikoani utakuta zinakataana.”
Neno linaloleta mushkeli hapa ni ‘kukataana’. Maana ya kukataa ni kusema au
kuonyesha kwa vitendo kutokubali jambo fulani , kusema hapana, kuzuia au
kunyima.
Sasa tunaposema kuwa takwimu zimekataana tuna maana ya kunyima, kuzuia au
kusema hapana. Maneno yote hayo hayaelekei kukaribia maana iliyokusudiwa.
Neno ambalo lingefaa hapa ni kutofautiana. Kwa maana hiyo, takwimu
zilitofautiana kati ya zile za wilayani na zile za mikoani.
Upo mtindo wa waandishi wa magazeti kuendelea kutumia neno maamuzi badala ya
uamuzi.
Angalia sentensi zifuatazo ambazo zimetokana na waandishi wawili tofauti na
katika nyakati tofauti:
“Haya ndiyo maamuzi magumu ya Pep Guardiala.”
“Hakika hakuna njia nyingine iwapo Jaji huyo, alitoa siri iliyoko kwenye
maamuzi kwa mtu mwingine wa pili”.
Kwa kuzingatia uandishi bora, maneno kama
maamuzi hayafai kuandikwa kwani yanakiharibu Kiswahili badala ya kukijenga.
Tuwe macho kutumia kamusi za Kiswahili ili kuwa na uhakika na kile tunachoandika.
“Askofu Telesphory Mkude alisema hakuna budi kwa Watanzania kuishi katika
maisha ya upendo na amani kama ambavyo Mungu
alikuwa anawafanyia watu wake.”
Matumizi ya ‘budi’ yanawakanganya watu wengi. Yafaa ieleweke kuwa tunapotumia
neno budi tuna maana ya hiyari lakini tunapolitumia hatuna budi, hapana budi,
sina budi, hawana budi tuna maana ya kusema ni lazima.
Kwa hiyo, ni muhimu kufahamu kuwa ukisema ni budi niende maana yake una
hiyari ya kwenda. Kama ukisema sina budi
niende maana yake ni lazima niende.
“Mungu amekuwa akimsamehe kila mtu dhambi zake hususani wale wanaotambua na
kumrejea kumwomba awasamehe.”
Kwa kawaida, maneno ya Kiswahili na hata yale yanayotoholewa, yanafuata
msingi wa lugha ya Kiswahili usemao kuwa ni lazima kuishia na irabu (a, e, i,
o, u).
Hata hivyo, tunayo maneno machache ambayo hayafuati kanuni hii. Maneno
haya ni kama takriban, mathalan, hususan,
marmar (marumaru). Orodha ya maneno haya ni fupi lakini ni muhimu kuyajua na
kuyatumia ipasavyo.
“Kamati yake inasisitiza kuwa halmashauri zote za Mkoa wa Lindi kutunga
sheria ndogo mpya kwa kutambua dhumuni la sheria hizo.”
Katika kipindi kilichopita niwahi kueleza kuwa yako maneno ambayo hayana
wingi bali yana umoja tu ijapokuwa neno lenyewe limeanza na kiambishi ma-.
Kwa mfano yako maneno kama maji, maradhi,
maumivu, madhumuni, maoni na kadhalika ambayo tunayatumia katika umoja
na wingi.
Katika Kiswahili hatuna maneno kama
radhi (maradhi), umivu (maumivu), dhumuni (madhumuni) au oni (maoni). Kama ukiyatumia watakushangaa wajuzi wa lugha ya
Kiswahili kwani umeipotosha lugha.
Kwa upande mwingine, tunayo maneno kama
ushirikiano na wala siyo mashirikiano, uamuzi na wala siyo maamuzi, shule na
wala siyo mashule, upungufu na wala siyo mapungufu, hospitail na wala siyo
mahospitali, hoteli na wala siyo mahoteli, benki na wala siyo mabenki,
kampuni na wala siyo makampuni
|
MAPISHI
‘FISH FINGER’
Karibu sana katika safu hii ya mapishi ambapo leo
ninakuletea upishi wa chakula kinachoitwa ‘ Fish Finger’. Ungana nami
mtayarishaji wako Cosmas Pahala.
1.
Samaki wakubwa
kiasi
2.
Nyanya 5
3.
Hoho 1
4.
Karoti 1
5.
Nyanya kopo 1
6.
Chumvi kiasi
7.
Vitinguu maji na
saumu
8.
Mafuta ya kupikia
9.
Pilipili 3
10.
Ndimu
Jinsi ya kupika
1.
Kausha vipande
vitatu vitatu kwa jua, vikisha kauka visage kwa kutumia blenda (kifaa maalum
cha kusagia), vikiwa tayari weak kwenye sahani.
2. Paka samaki
wako chumvi, twanga vitunguu saumu uweke samaki, tia ndimu na maji
kiasi.kwenye
3. Bandika jikoni acha yachemke mpaka maji yote
yachemke. Toa miiba ya samaki.
4.
Changanya samaki
wako mpaka wachanganyike kabisa kasha viringisha vipande vipande kama vidole.
5.
Weka kwenye ule
unga wa mkate ulio kwisha usaga, vunja mayai na tumbukiza vipande kwenye mayai.
6.
Weka mafuta
jikoni yapate moto tumbukiza ‘fish finger’ zako ambazo ulizipaka unga wa mkate
na mayai.
7.
Acha mpaka ziwe
na rangi ya kahawia na uzitoe na kuziweka kwenye chombo kisafi, na hapo
zitakuwa tayari kwa kuliwa.
SHAIRI
MISAADA
YA WAGENI
Wazungu
wanayo nongwa, Haki wanatudhulumu
Wanaleta
ya paukwa, Twabaki mashamusham
Kila
tunacholetewa, Mwishowe twajilaumu
Misaada
ya wazungu, Ona inavyo tutesa.
Serikali
kuelewa, Hii inawalazimu
Misaada
mnayopewa, Ndani ndani yake kunabomu
Tusipende
vya kupewa, Tukumbuke ya mwalimu
Misaada
ya wazungu, Ona inavyotutesa.
Kanisa
tumeambiwa, Hii ni ya kwetu zamu
Mitumba
tunaletewa, Na fedha za kujikimu
Majengo
tunajengewa, Ila hili tuheshimu
Misaada
ya wazungu, Ona inavyo tutesa.
Ndoa
ya jinsia sawa, Zifungishwe kwa hakimu
Ndoa
ya jinsia sawa, Ati yaitwa karamu
Mwanaume
sawasawa, Kuolewa si haramu?
Misaada
ya wazungu, Ona inavyo tutesa.
Mashehe
wetu wazawa, Nawachungaji hudumu
Hii
ni chemsha kinywa , Sasa ni yakwetuzamu
Wazee
kwetu ni dawa, Tunusuruni kaumu
Misaada
ya wazungu, Ona inavyo tutesa
HUYU NDIYE RAIS TUNAYE MUHITAJI
DSJ
Usomi wa ngazi mbalimbali si
sifa ya mtu kufaa kuwa kiongozi, dunia katika historia yake ina majina lukuki
ya baadhi ya viongozi ambao walikuwa wasomi, lakini hatima ya uongozi wao
haikutofautiana na wajinga.
Hata hapa nchini kuna baadhi ya viongozi serikalini, kwenye mashirika na hata
kwenye sekta binafsi ambao wakikuonesha vyeti vyao vya shule unaweza kuogopa,
lakini utendaji wao ni kichefuchefu.
Tukiwa tunaelekea katika
uchaguzi mkuu wa viongozi wa serikali ya wanafunzi (DASJOSO), wanafunzi wa DSJ
wanatakiwa kuangalia kiongozi ambaye ataweza kuisogeza mbali serikali ya
wanafunzi (DASJOSO) na mwenye uono wa
mbali kwa maendeleo ya serikali na chuo kwa ujumla.
Kisaikolijia sifa za kiongozi ziko wazi na ni muhimu, mtu kuwa nazo kabla au
baada ya kupewa cheo. Leo tunataka kuziangalia kwa undani sifa hizi, ili kama wanafunzi
wenye dhamana ya kuchagua watu wa kuongoza tuwatazame watu kwa sifa zao
kabla na baada ya kuwapa nafasi. Sifa za kiongozi ni hizi zifuatazo:
Awaze mafanikio makubwa
Raisi wa Dasjoso lazima awe na maono ya juu ya kuhakikisha kuwa , serikali ya
wanafunzi inapata mafanikio makubwa, hii ndiyo itakuwa dira ya kazi yake
itakayompa muongozo wa kusimamia
watendaji wote walio chini yake kufikia kiwango cha mafanikio
anachokiwaza. Kiongozi asiyekuwa na mawazo ya juu ya kuendelea kutoka mahali
alipo hafai kuongoza.
Awe na nia
Haitoshi kwa Rais kuwa na mawazo chanya peke yake bila kuwa na nia ya
kuyatimiza. Hivyo, Rais atafaa kuchaguliwa kuwa kiongozi endapo tu atakuwa na
uwezo wa kuratibu vema na kutekeleza alichowaza. Ajue njia anayopita,
awatangulie anaowaongoza kwa vitendo.
Ajitambue mwenyewe
Lazima kiongozi ajitambue mwenyewe ni mtu wa namna gani, ajue uwezo wake na
upungufu wake na awe tayari kujiongezea maarifa kila siku, ili aweze kukabili
changamoto na mabadiliko ya ulimwengu. Asome, afuatilie mambo yanavyokwenda na
ajifunze kwa wenzake kuhusu kufanikisha malengo yake.
Asimamie maamuzi
Kuna wakati malengo hukumbana na vikwazo, hivyo ni wajibu wa Rais kusimamia
maamuzi sahihi na kuwa mtu wa mwisho. Kiongozi mwenye kubadilika badilika kama kinyonga, hafai kwa vile kukosa msimamo kuna
maanisha udhaifu wa mipango na kujiamini.
Adhibiti msongo wa mawazo
Tunamtarajia kiongozi mzuri awe ni mtu mwenye kupunguza msongo wa mawazo, ili
kuifanya akili yake ifikie maamuzi sahihi, lakini kama
atakuwa mwenye kuwaza mengi, atajikuta anachanganyikiwa na kuwa mtu wa jazba
katika maamuzi na hivyo kuipotosha jamii.
Akubali kukosolewa
Viongozi wasiokuwa na sifa za uongozi huwa hawakubali kukosolewa, wakidhani
kuwa hiyo ndiyo njia ya kuthibitisha msimamo wao na usahihi wao. Kiongozi
makini ni yule ambaye atakuwa tayari kukosolewa na kuwapongeza wanaomkosoa kwa
kutazama mwenendo wake na usahihi wake. Asiyekubali kukosolewa hafai kuwa
kiongozi.
Awe msikilizaji
Rais mzuri ni yule ambaye atakuwa tayari kuwasilikiza watu walio chini yake,
apokee maoni yao
na ikiwezekana ayafanyie kazi. Lakini pia anatakiwa kuwafahamu kwa undani, ili
aweze kuwaongoza vema kufuatana na hali zao. Akiwa na watu walemavu wenye
kasoro kadhaa wa kadhaa anatakiwa kuwatambua kabla na baada ya kuwa kiongozi
wao. Kuongoza usichokifahamu ni ujinga.
Afuate haki
Kiongozi imara anatakiwa kufuata haki katika kuongoza kwake, asijione mwenye
haki zaidi ya wale anaowaongoza katika sheria. Ni muhimu kwake kuwafanya walio
chini yake kujiona wako huru katika mawazo na matendo. Kiongozi anayetumia
nguvu na ukali kuongoza watu hafai. Hata yule mwenye kujivunia uongozi wake
naye hafai.
Awe egemeo la watu
Sifa nyingine ya rais ajaye awe egemeo la watu wake katika shida na raha.
Kiongozi mzuri ni yule ambaye atakuwa tayari kusikitika, kuomboleza, kufurahi
pamoja na watu wa chini yake bila kujitenga nao. Ajitolee kuwatumikia watu kwa
hali na mali
na awe tayari kutumika zaidi kwa maslahi ya wengine.
Atie moyo watu
Raisi wa DASJOSO ajaye anatakiwa
kuwa na uwezo wa kuwatia moyo walio chini yake ili waweze kuendeleza vipaji
vyao. Haipendezi kwa kiongozi kuwavunja moyo watu kwa kauli za kudharau kazi na
jitihada zao walizojaribu kufanya katika kutekeleza majukumu yao
kama wafanyakazi au wananchi.
Afurahie mafanikio
Sifa nyingine muhimu ya Rais tunaye mtaka awe tayari kufurahia mafanikio
aliyopata pamoja na watu wake. Ni wajibu wa kiongozi kutoa tuzo, kuwashukuru
wafanyakazi wake na kuwa tayari kuwapa ofa. Hii itasaidia kuwafanya watu waone
hawajapoteza nguvu zao katika utendaji wao na kwamba wanakubalika. Si busara
wakati mwingine kuwakosoa watu mbele ya hadhara na kueleza kutofurahishwa na
kazi zao.
Aungane na wa chini yake
Mtu kuwa Rais haimaanishi amekuwa wa tofauti na watu wengine kiasi cha
kushindwa kuchangamana nao kama wanavyofanya
baadhi ya viongozi. Rais mwema ni yule atakayeungana na watu wake katika maisha
ya kawaida. Kuwa kiongozi haimaanishi kwamba watu watakufuata wewe kila siku,
wakati mwingine wewe unatakiwa kuwafuata wao na kuwa nyuma yao hata mahali walipokosea au wanapokabiliwa
na makosa, watetee na uoneshe kuwajali na kuwapigania, makosa utayahesabu baada
ya utetezi wako kukamilika.
Akubali lawama
Kama Rais akifanya mambo ambayo jamii haikupendezwa nayo anachotakiwa kufanya
ni kukubali kulaumiwa. Ikiwa anaongoza kitego cha umeme kwa mfano na watu
hawakupata nishati hiyo kwa wakati hatakiwi kukwepa lawama, vivyo hivyo kwenye
wizara na idara au nchi kwa ujumla.
Afahamu kutatua matatizo
Raisi tunaye mwitaji ni yule ambaye atakuwa na uwezo wa kuzuia migogoro na
kuitatua kwa haraka. Muongozo mzuri katika eneo hili umesimama katika
mawasiliano na watu wa chini, mawasiliano haya ndiyo yatakayomuwezesha kiongozi
kujua matatizo waliyonayo wafanyakazi wake au hata jamii anayoiongoza na hivyo
kumfanya apate wasaa wa kuyashughulikia mapema.
Ajifunze kwa makosa
Wakati mwingine mawazo na mipango inaweza ikaenda kombo, hivyo ni wajibu wa
Rais atatakiwa kujifunza kutokana na makosa yake au ya wale anaowaongoza, ili
kuepuka kurudia makosa yale yale na kumfanya apoteze sifa za kuwa kiongozi
mzuri.
Mwanafalsafa Winston Churchill aliwahi kusema "The price of greatness is
responsibility." Thamani ya ukuu ni uwajibikaji.
Awe mwaminifu
Miongoni mwa maeneo magumu kabisa yaliyowashinda na yanayoendelea kuwashinda
viongozi wengi ni uaminifu. Rais wa DASJOSO anatakiwa awe tayari kusimamia
muongozo wa katiba ya nchi au marufuku alizowekewa katika madaraka yake. Hii
inakwenda sambamba na kutowaonea, kuwanyanyasa wa nchini yake kwa kutumia cheo
chake.
Awe mkweli
Viongozi wengi hasa wa kisiasa siku hizi ni waongo hakuna mfano, wamejaa ahadi
zisizotekelezeka na hata wanapogundua kuwa hawana uwezo au wamekwama
kuzitimiza, hawaoni haja ya kutubu mbele ya wanaowaongoza. Kiongozi makini ni
yule atayekuwa tayari kuonesha ubora wa matendo na kauli zake.
Asiwe mwenye majungu
Kuna baadhi ya viongozi kwenye maofisi wanaendekeza sana majungu na pengine kuyapa umuhimu wa
hali ya juu. Hii ni sifa mbaya kwa kiongozi yo yote, hivyo anayetumikia ‘umbea’
katika ofisi aliyokabidhiwa kama mkuu anapaswa
kuondolewa. Kiongozi makini atatumia uwezo wake kuzuia watu
wasimsengenye/wasisengenyane kwa kuwa muwazi na mwenye kufungua milango ya watu
kumuona na kumlaumu na kueleza hisia zao.
Awe bora
Kwa kila analofanya kama rais lazima alifanye
kwa ubora, asiwe mtu mwenye kulipua kazi na kufanya chini ya kiwango cha uwezo
wake. Kila siku katika kazi, maamuzi, usimamizi, utekelezaji lazima atumike
zaidi ya uwezo wake.
Nguzo imara ya mwanafunzi yeyote anayetaka kufanikiwa katika masomo yake ni
kuwa mfuasi wa UTII na UAMINIFU mahali popote na kwa mtu yeyote. Nakumbuka
wakati nikiwa shule ya sekondari nilikiuka
sana mambo haya muhimu, nilikuwa mtu wa
vurugu na mwanzilishi wa migomo.
DALILI KUMI NA TATU ZA MIMBA
Na
Cosmas Pahalah
MWANAMKE anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za
kawaida. Na ni wakati huo ambao ni muafaka kwake kuanza kuuchunguza mwili wake.
“Homoni zinazosambaa mwilini mara tu unapopata ujauzito husababisha mabadiliko
kadhaa katika mwili wake ambayo yanaweza kugundulika kabla hata ya uchunguzi
halisi wa kujua kama mjauzito au la,” anasema Melissa Goist, Profesa na
Mtalaama wa Masuala ya Uzazi wa Chuo Kikuu cha Ohio, Marekani.
Maumivu kwenye matiti
Hii ni dalili ya kawaida ya ujauzito ambapo nguvu za homoni mwilini huongezeka
wakati yai linavyopata “rutuba”, jambo ambalo huongeza wingi wa damu na
kuyafanya matiti ya mwanamke kuvimba na kuwa makubwa isivyo kawaida.
Maumivu mwilini
Utaanza kusikia maumivu kama vile unataka
kuingia katika siku zako. Kwa kawaida hali hii hutokea wakati yai likiwa
linasafiri kwenda katika chumba cha mimba. Hivyo, hali hiyo husababisha sehemu
hiyo itanuke taratibu na kusababisha maumivu hayo.
Kutokwa damu bila kutegemea
"Wanawake wengi hufikiria kutokwa na damu kidogo ni dalili ya kuwa katika
siku zao. Lakini, katika hali halisi, kutokwa damu kusikotegemewa, huwakumba
asilimia 25 ya wanawake wakati wa kurutubika kwa yai,” anasema Goist. Ambaye
anaendelea kusema kwamba iwapo utaona hedhi yako inakuwa fupi au inafanyika
katika hali ambayo si ya kawaida, unashauriwa kwenda kufanya kipimo cha
ujauzito..
Kuchoka
Unapojisikia kuchoka na kukosa raha, au kutaka hata kulala wakati ukiwa kazini,
lazima ufahamu kwamba mwili wako unajirekebisha kuingia katika kipindi kipya
cha mabadiliko.
“Tambua kwamba katika kipindi cha mwanzo cha ujauzito ni muda ambao mtoto
tumboni huanza kutumia sehemu ya nguvu zako na hivyo kukuletea uchovu na
usingizi” anasema Goist.
Chuchu kuwa nyeusi
Chuchu huanza kubadilika rangi yake kutokana na chembechembe za uhai (seli)
kuanza kufanya kazi kwa nguvu zaidi. Hata hivyo, Goist anasema: “Wanawake wenye
ngozi nyeusi hawawezi kuiona dalili hii mapema hadi muda wa kama
wiki kumi zipite.”
Kichefuchefu
Hali hii huwapata asilimia 85 ya wanawake wanapopatwa na ujauzito, ambapo
nyakati za asubuhi ndipo hasa hujionyesha.
Mwili kuvimba
Kuna wakati kupungua kwa nguvu za uyeyushaji chakula kunaweza kukusababishia kuona
tumbo limevimba na nguo zikawa zinakubana kutokana na chakula kujaa katika
utumbo. Lakini hali hiyo ikiendelea na ukaona siku zako haziji, basi ni vyema
ukatambua kwamba tayari una ujauzito na kinachokupasa ni kwenda kuhakikisha.
Kwenda haja ndogo mara kwa mara
Kwenda haja ndogo kila mara ni dalili kwamba kibofu chako kimeanza kufanya kazi
ya ziada, ambapo huwa kinafanya kazi ya kuondoa maji kwa uthabiti zaidi wakati
wa ujauzito. Hali hii pia hujitokeza mwishoni mwa ujauzito, ambapo kibofu
kitakapokuwa kinarudia hali yake ya kawaida baada ya kufanya kazi kwa muda
mrefu.
Tamaa ya vitu mbalimbali
Kutokana na mwili kuwa na “mzigo” wa ujauzito na hivyo kuchoka, hali hiyo
humfanya mwanamke kutamani vitu mbalimbali ili kukidhi mabadiliko
yaliyojitokeza katika mwili wake. Hii ni pamoja na kutaka vyakula fulani au
kufanya mambo ambayo hapo nyuma alikuwa hayapendi.
Kuumwa kichwa
Kuongezeka kwa damu kunaweza kusababisha kichwa kuuma japokuwa si sana, hususani katika wiki
za mwanzo za ujauzito. Hata hivyo, hali hii hukoma mwili unapojirekebisha na
mzunguko wa homoni unaotokana na ujauzito.
Kufunga choo
Homoni ambazo husababisha mwili kuvimba pia husababisha kufunga choo kutokana
na mfumo wa kuyeyusha chakula kutofanya kazi vyema. Hata hivyo hali hii inaweza
kujitokeza zaidi wakati ujauzito unapoendelea kukua.
Kuwa na hasira
"Kutokana na kuongezeka kwa homoni za utendaji kazi mwilini, hali hiyo
itakusababishia uchovu, na kukufanya kuwa na hasira,” anasema Goist
Kuongezeka kwa joto mwilini
Kipimo cha joto la mdomo ni muhimu katika kutambua hali ya ujauzito. Kwa
kawaida joto huongezeka kwa nyuzi moja au zaidi wakati yai likiwa linatunga
mimba. Hali hiyo ikiendelea kwa zaidi ya wiki mbili, itakuwa inaonyesha dhahiri
kwamba kuna “mtoto anakuja”.