Na Cosmas J. Pahalah
Wataalamu wa afya ni nyenzo muhimu
katika maisha yetu ya kila siku kutokana na mchango wao kutibu magonjwa
mbalimbali kwenye miili yetu
Ili tuweze kutimiza hadhima yao wadau,Serikali na
taasisi mbalimbali Nchini zinatakiwa ziwaunge mkono kwakutambua umuhimu wa kazi
zao ili waweze kusogeza huduma hizo kwa Wananchi.
Dkt Kefa Omary kutoka kituo cha Medical
Missionaries Lifestyle centre ni mmoja katia ya wataalamu wanaotibu magonjwa zaidi ya kumi kwa kuwaelimisha
Wananchi juu ya umuhimu wa kula matunda,juisi pamoja na chakula bora ili
waepukane na magonjwa nyemelezi kwenye miili yetu.
Anasema kuwa huduma hiyo yakuwaelimisha
Wananchi juu ya umuhimu wa kula vyakula bora wanaitoa bure kwa Wananchi ikiwa
ni moja kati ya mipango mikakati ya kituo hicho.
Hata hivyo anasema kuwa magonjwa
anayotibu na kwakuwaelimisha Wananchi juu ya umuhimu wa kula vyakula
bora,pamoja nakufuata sheria nane za Afya(NEWSTART). Baadhi ya magonjwa anayo
yatibu ni vidonda vya
tumbo,kisukari,saratani,presha yakupanda na kushuka,pamoja na matatizo ya
uzazi,kiarusi,figo,prostrate,macho, kifafa, fungus, ini ,chango, pumu na
kupunguza unene.
Anasema kuwa Kituo hicho kinatoa elimu
kupitia makanisa,shule,vyuo ili kuleta hamasa kwa Wananchi kujua umuhimu wa
kula vyakula,juisi pamoja na matunda ili waepukane na magonjwa ya mlipuko.
Pia hutoa elimu kupitia
makongamano na maonesho mbalimbali ndani na nje ya nchi, kama vile
maonesho ya sabasaba, na kongamano la vijana katika chuo kikuu cha Sokoine
nakatika chuo kikuu cha Rwanda,
BARATON kilichopo nchini Kenya.
Hata hivyo anasema kuwa katika
kuhakikisha huduma hiyo inawafikia Wananchi kituo kinategeme Chuo
kitakachojulikana kwa jina la Medical Missinaries Life Style Centre kutoa elimu
kwa wananchi
“Taasisi yetu ipo chini ya chuo cha
Lomalinda kilichopo nchini Marekani; pia kuna matawi mengine ambayo ni chuo cha
Kibidura kilichipo Iringa pamoja na
River side kilichopo Zambia,
ikiwa ni moja ya harakati zetu katika kuhakikisha elimu hii ya kula vyakula
bora pamoja na juisi inawafikia Wananchi”.
Anasema kuwa licha ya kituo hicho kutoa
elimu juu ya umuhimu wa kula vyakula bora, pia kinajishughulisha na uelimishaji
Wananchi juu ya ugonjwa wa ukimwi.
``Sisi wenyewe ni mashahidi,tumejionea
jinsi gani nguvu ya Taifa inavyopotea kutokana na nguvu kupungua hivyo basi
sisi kama wataalamu wa afya tumeamua kusimama kidete katika kuwaelimisha
Wananchi juu ya madhara yatokanayo na ugonjwa wa ukimwi ili nguvu kazi ya Taifa
isipotee``anasema,Dkt Kefa.
Hata hivyo anasema kuwa elimu juu ya madhara
yatokanayo na ukimwi wamekuwa wakiitoa kupitia warsha na makongamano mbalimbali
Nchini,mashuleni na Vyuo vyote Nchini ili iwe rahisi kusambaa kwa wengine.
Anasema kuwa baada ya kituo hicho kutoa
elimu ya madhara ya ugonjwa wa ukimwi kwa wananchi wamekuwa na tabia
yakuwatembelea Wananchi mara kwa mara ili kujua kama elimu kama
imewafikia Wananchi.
``Tumekuwa na tabia ya kuwatembelea
Wananchi wetu mara kwa mara ili kujua kama elimu imewafikia,nini kifanyike,wapi
hawajaelewa ili wajiepushe na ugonjwa wa ukimwi.
Anaongeza kuwa kituo hicho pia ni
sehemu moja wapo kwa Wananchi kujipatia ajira kutokana na kutoa elimu kwa
wanaohitaji ili nao waanzishe vituo vyao.
Anasema kituo hicho kimeweza kutoa
wataalamu mbalimbali kutokana na wengi wao kujua namna ya kupika, na kuandaa
juisi mbalimbali kama juisi ya karoti ambayo
wamekuwa wakiiuza ili wajipatie vipato vyao vya kila siku.
Dkt Kefa anasema kuwa kituo hicho
kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo vifaa vya kutolea huduma pamoja na
uwezo wakuwalipia vipindi vitakavyowaelimisha Wananchi juu ya umuhimu wa kula
vyakula bora,matunda,juisi ili waepukane na magonjwa ya mlipuko.
``Ninajitahidi elimu hii iwafikie
Wananchi wangu kwa ukaribu na kwa urahisi,lakini ninaomba Serikali wadau na
taasisi mbalimbali Nchini ziniunge mkono ili elimu hii iwafike kwa
urahisi``anasema,Dr Kefa.
Anaomba Serikali wadau na taasisi
mbalimbali Nchini zimuunge mkono kwakukisaidia kituo hicho fedha za kugharamia
vipindi kwenye vyombo vya habari ili elimu hiyo ifike Tanzania nzima.
``Ninataka wakati sasa ufike hata
Mwananchi aliyeko kijijini ajue juu ya umuhimu wa kula matunda ili wajiepushe
na magonjwa nyemelezi katika miili yao,lakini
yote haya yanawezekana kama tukipata fedha za
kununu vipindi kwenye vyombo vyetu vya habari ili elimu hii iwafike
Wananchi``anasema,Dkt Kefa.
No comments:
Post a Comment