Yesu ni Muhimu Leo?
Kwanini
Yesu?
Wengi wanafikiri kwamba Yesu Kristo
anataka kuwa mtu wa dini. Wanafikiri Yesu alikuja kuondoa raha zote katika
maisha, na kutupa sisi taratibu zisizowezekena tuishi nazo. Wako tayari kumwita
ni kiongozi mkubwa wa tangu zamani, lakini wanasena yeye si muhimu kwa maisha
yao leo.
Josh McDowell alikuwa ni mwanafunzi
wa chuo aliyefikiria Yesu alikuwa kiongozi mwingine wa kidini aliyeweka
taratibu zisizowezeka kuishi pamoja nazo. Alifikiri Yesu alikuwa si muhimu
kabisa kwa maisha yake.
Kisha siku moja katika mjumuiko wa
wanafunzi katika meza ya chakula cha mchana. McDowell aliketi karibu na kijana
mchangamfu aliye na tabasamu kubwa . Akiwa ameamsha hamu ya kudadisi,
akamwuliza kwanini alikuwa mwenye furaha sana. Jibu lake la haraka lilikuwa,
“Yesu Kristo”
Yesu Kristo? McDowell akasirika, akarudishia swali tena:
“Oh, Kwa haki ya Mungu, usiniletee
mimi huo upuuzi. Nimechoshwa na dini; Nimechoshwa na kanisa; Nimechoshwa na
Biblia. “usiniletee mimi huo upuuzi kuhusu dini.”
Lakini kijana ambaye hakushangazwa
kwa utulivu akamtaarifu,
“Bwana, sikusema dini, nimesema Yesu
Kristo.”
McDowell alishangazwa. Hakuwahi
kumfikiria Yesu zaidi ya mtu wa dini, na hakutaka sehemu yoyote ya unafiki wa
kidini. Lakini bado hapa palikuwa na mwanamke mkristo akimzungumzia Yesu kama
mtu fulani ambaye amemletea maana kwa maisha yake.
Kristo alidai kujibu maswali yote ya
kina kuhusu kuwapo kwetu. Katika wakati mmoja au mwingine, wote tunauliza ni
kitu gani maisha yapo kwacho. Umewahi kuangaza kwenye nyota wakati wa jioni ya
giza jeusi na kujiuliza nani ameziweka pale? Au umewahi kuona kuzama kwa jua
(mawio) na kufikiria kuhusu masuala makubwa ya maisha:
- “Mimi ni nani?”
- “Kwani nipo hapa?”
- “Wapi ninakwenda baada ya kufa?”
Ingawa wanafalsafa wengine na
viongozi wa dini wametoa majibu yao kwa maana ya maisha, Yesu Kristo pekee
amethibitisha uwezo wa mamlaka yake kwa kufufuka toka wafu. Wakosozi/wakosoaji
kama McDowell ambao tangu mwanzo walidharau (Saa Yesu Alifuka Wafu)
wamegundua kuna ushahidi unaothibitisha kwamba ni kweli ilitokea.
Yesu anatoa maisha yenye maana ya
kweli. Alisema maisha ni zaidi ya kupata fedha, kufurahi, kuwa na michezo, kufanikiwa
na kisha kuishia makaburini. Lakini bado watu wengi wanajaribu kutafuta maana
katika umaarufu na mafanikio hata watu maarufu wakubwa…
Madonna alijaribu kujibu swali la “Kwanini nipo hapa?’ kwa kuwa mwimbaji mwanamke maarufu, akikiri, “Kumekuwa na miaka mingi wakati ambapo nilifikiri umaarufu, bahati, heri na kukubaliwa na halaiki kungeniletea furaha. Lakini siku moja unaamka na kutambua hazileti [furaha]…. Nilihisi kitu fulani kilikuwa kinakosekana…. Nilitaka kujua maana ya furaha ya kweli idumuyo na jinsi gani ningeweza kwenda kuipata.”[1]
Wengine wamekata tamaa katika kutafuta maana. Kurt Cobain, mwimbaji mwongozaji wa bendi ya Seattle ya Nirvana, alikata tamaa ya maisha katika umri wa miaka 27 na akafanikisha kujiua. Mtaalamu wa vikatuni wa enzi ya muziki wa Jazz Ralph Barton pia aliona maisha kuwa hayana maana, akaacha kimeseji cha kujiua: “Nimepata shida chache, marafiki wengi, mafanikio makubwa; nimepitia toka mwanamke mmoja hadi mwingine, nyumba hadi nyumba, nimetembelea nchi za dunia, lakini nimechoshwa na kazi ya kuendelea kubuni vifaa muda wote wa saa 24 za siku nzima.”[2]
Pascal, mwanafalsafa mkubwa wa kifaransa aliamini huu uwazi ambao wote tunakabiliana nao unaweza tu kukamilishwa na Mungu. Anaeleza, “Kuna uwazi wa Mungu katika moyo wa kila mtu ambao Yesu Kristo peke yake anaweza kuujaza.”[3] Ikiwa Pascal yuko sawa, basi tungemratajia Yesu si tu kujibu swali la utambulisho wetu na maana katika maisha haya, lakini pia anatupa tumaini kwa maisha baada ya sisi kufa.
Kunaweza kuwa na maana, bila Mungu? Si kulingana na asiyeamini Mungu Bertrand Russell, aliyeandika, “labda uchukulie kuna mungu, suala la madhumuni ya maisha halina maana.”[4] Russell alijuzulu mwenyewe mwishowe kwa ku”oza” kaburini. Katika kitabu chake, Kwanini mimi si mkristu, Russell alitupilia mbali kila kitu Yesu alisema kuhusu maana ya maisha, ikiwamo ahadi yake ya uzima wa milele.
Lakini ikiwa Yesu kwa kweli alishinda kifo kama mashahidi wa macho walivyodai, (Saa Yesu Alifufka Wafu) basi ni yeye mwenyewe angeweza kutuambia nini maisha yapo kwa sababu, na kujibu “Wapi ninaenda?” ili kuelewa jinsi gani maneno ya Yesu, maisha na kifo yanaweza kuimarisha utambulisho wetu kutupa maana katika maisha, na kutoa matumaini kwa siku zijazo, tunahitaji kuelewa kitu gani alisema kuhusu Mungu, kuhusu sisi na kuhusu yeye mwenyewe.
Yesu alisema kitu gani kuhusu Mungu?
Mungu ni wa busara
Wengi wanamfikiria Mungu zaidi kuwa kama nguvu fulani kuliko mtu tunayeweza kumwona na kumfurahia. Mungu ambaye Yesu alimzungumzia si kama nguvu isiyo ya kinafsi katika mvutano wa nyota ambayo uzuri wake unapimwa kwa volti. Wala is roho mwovu mkubwa asiye na huruma angani, akipendezwa kufanya maisha yetu ya huzuni.Kwa kinyume, Mungu ni wa busara kama sisi, lakini hata zaidi ya hapo. Anafikiri, anasikia. Anazungumza katika lugha tuyonaweza kusikia. Yesu alituambia na alituonyesha namna Mungu alivyo kama. Kulingana na Yesu, Mungu ajua kila mmoja wetu, kwa siri na binafsi, na anaendelea kutufikiria sisi siku zote.
Mungu anatupenda
Na Yesu alituambia kwamba Mungu anatupenda. Yesu alidhihirisha upendo wa Mungu pote alipoenda, wakati alipowaponya wagonjwa na aliwafikia wanaumizwa na maskini.Upendo wa Mungu ni tofauti kabisa na wetu na kwa huo (upendo) haujajengwa kutokana na mvuto au utendaji kazi. Ni wa sadaka kwa ujumla na si mbinafsi. Yesu alilinganisha upendo wa Mungu na upendo wa baba mkamilifu. Baba mzuri anataka mazuri zaidi kwa watoto wake, anajitoa sadaka kwa ajili yao na anawapatia mahitaji. Lakini kwa faida zao zaidi, anawaadabisha.
Yesu anaelezea moyo wa Mungu wa upendo kwa hadithi kuhusu kijana muasi ambaye alikataa ushauri wa baba yake kuhusu maisha na kile kilicho muhimu. Akiwa mwenye kiburi na nia binafsi, kijana alitaka kuacha kazi na “kuishi maisha ya anasa na starehe”. Kuliko kusubiri hadi baba atakapokuwa amekuwa tayari kumpa urithi wake, alianza kusisitiza kwamba baba yake ampe mapema.
Katika hadithi ya Yesu, baba alimpatia kijana wake ombi lake. Lakini mambo yalienda vibaya kwa kijana. Baada ya kuponda fedha zake kwa starehe binafsi, kijana muasi ilimbidi kuenda kufanya kazi katika shamba la nguruwe. Muda si mrefu alikuwa na njaa hata chakula cha nguruwe kilionekana kizuri kwake. Akiwa amekata tamaa na matumaini asiye na uhakika baba yake angemkubali arudi, alipakia begi lake na akaelekea nyumbani.
Yesu anatuambia kwamba sio tu baba yake alimkaribisha nyumbani, lakini kwa kweli alimkimbilia na kukutana naye kumpokea. Na kisha baba yake alipatwa na upendo mkuu na akafanya sherehe kusherehekea kurudi kwa mtoto wake.
Inafurahisha kwamba ingawaje baba alimpenda kijana wake sana, hakumfuatafuata. Alimruhusu kijana aliyempenda ausikie uchungu na atesekee matokeo ya uchaguzi wake wa uasi. Katika namna ya kufanana, maandiko yanafundisha upendo wa Mungu hautaacha/hautalegeza kamba kwa kile kilicho bora kwetu. Yataturuhusu kusotea matokeo ya chaguzi zetu zisizo sahihi.
Yesu pia alifindisha kwamba Mungu hatalegeza kamba kwa tabia yake. Tabia ni vile sisi tulivyo kwa ndani zaidi. Ni asili yetu ambapo mawazo yetu yote na matendo yetu yanaanzia. Kwa hiyo Mungu yupo kama nani -kwa ndani zaidi?
Mungu ni Mtakatifu
Kote katika maandiko (karibu mara 600), Mungu anazungumziwa kama “mtakatifu”. Mtakatifu inamaanisha kwamba tabia ya Mungu ni safi kiroho na kamilifu kwa kila njia. Isiyo na kasoro. Hii inamaanisha kwamba haendekezi fikra ambayo ni chafu au ambayo haiendani na ubora wake kiroho.Zaidi ya hapo, utakatifu wa Mungu unamaanisha kwamba hawezi kuwa malipo na uovu. Kwa sababu ubaya ni kinyume na asili yake, anauchukia. Ni kama uchafu kwake.
Lakini ikiwa Mungu ni mtakatifu na anachukia uovu, kwanini hakufanya tabia zetu ziwe kama zake? Kwanini kuna wanajisi-watoto, wauaji, wabakaji na wapotofu? Na kwanini tunapambana hivyo kwa chaguzi za mioyo yetu? Hiyo inatupeleka kwenye sehemu nyingine ya kutafuta kwetu maana. Nini Yesu alisema kuhusu sisi?
Nini Yesu alisema kuhusu sisi?
Tumeumbwa kwa ajili ya uhusiano na Mungu
Ungesoma Agano Jipya, ungegundua kwamba Yesu aliendelea kuzungumzia thamani yetu kubwa kwa Mungu, akituambia kwamba Mungu alituumba sisi kuwa watoto wake.Muairishi wa U2 rock star Bono alisema kwenye mahojiano, “ni wazo la kushangaza kwamba Mungu aliyeumba Ulimwengu angekuwa anahitaji kampani, uhusiano wa kweli na watu….”[5] Kwa maneno mengine, kabla ya ulimwengu haujaumbwa, Mungu alipanga kutulea sisi kuwa familia yake. Sio hivyo tu, lakini alipanga urithi wa ajabu kwamba ni wetu sisi kuuchukua. Kama ilivyo moyo wa Mungu baba katika hadithi ya Yesu, Mungu anataka kutuweka sisi katika urithi wa baraka zisizofikirika na faida ya utukufu. Katika macho yake, sisi ni maalumu.
Uhuru kuchagua
Katika sinema ya wake wa Stepford, wadhaifu, wamelala, waroho na wanaume wauaji wametengeneza roboti tiifu, nyenyekevu kuwaondoa wanawake wao waliohurishwa ambao wanawafikiria kuwa vitisho. Ingawaje wanaume wanapaswa kuwapenda wake zao, wamewadharau kwa ajili matoi ili kulazimisha utiifu wao.Mungu angeweza kutuumba kama hivyo – watu kama roboti (watu-mtambo) tukalazimishwa kumpenda na kumtii, akapangilia ibada ndani yetu kama pazia la skrini. Lakini upendo wetu wa lazima ungekuwa hauna maana. Mungu alitutaka sisi tumpende Yeye kwa uhuru. Katika mahusiano ya kweli, twataka fulani atupende tulivyo, si kwa lazima – tungependelea mwali/msichana mwenzi wa roho zaidi ya mwali wa kutumwa kama barua. Søren Kierkegaard aliandika kwa kifupi kutangatanga katika hadithi hii.
Fikiria kungekuwa na mfalme aliyependa mjakazi mnyenyekevu. Mfalme huyo angekuwa kama vile hakuna mwingine wa mfano. Kila kiongozi angetetemeka mbele ya mamlaka yake… na bado mfalme huyo mwenye nguvu alilainishwa na penzi la mjakazi mnyenyekevu. Namna gani angetangaza penzi lake kwake? Katika namna isiyo ya kawaida, ufalme wake ulifunga mikono yake. Angemleta mbele ya jumba la kifalme and kumvisha taji kichwa chake pamoja na johari… asingekataa – hakuna aliyethubutu kumbishia. Lakini angempenda yeye (mfalme)? Angesema amempenda bila shaka, lakini angempenda kikweli?[6]
Unaona tatizo. Kwa uhalisia kidogo tuseme: Unaachanaje na mvulana-rafiki anayejua yote? (“Si tatizo kati yetu, lakini nafikiri tayari unajua hilo”) Lakini ili kuumba upendo unaweza kupeana kwa uhuru, Mungu aliumba binadamu wenye uwezo wa pekee na nia huru.
Uasi dhidi ya Sheria za Maadili za Mungu
C.S. Lewis alitoa sababu kwamba ingawaje ndani tumeumbwa na hamu kumjua Mungu, tunaasi dhidi yake tangu kipindi tunazaliwa.[7] Lewis pia alianza kuchunguza vichocheo vyake mwenyewe ambavyo vilimwongoza kwenye ugunduzi kwamba kwa hulka-asilia alijua mema mbali na mabaya.Lewis alijiuliza wapi fahamu hii ya mema na mabaya ilitoka. Wote tunaisikia fahamu hii ya mema na mabaya wakati tunaposoma Hitler akiuua wayahudi milioni sita, au shujaa akijitoa akitoa sadaka maisha yake kwa ajili ya mtu fulani. Kwa hulka-asili tunajua ni vibaya kusema uongo na kudanganya. Kutambua huku kwamba tumetengenezwa pamoja na sheria ya ndani ya maadili kulimfanya mwamini miungu wa mwanzo afikie hitimisho kwamba lazima kuna “mtoa sheria ya maadili.”
Hasa, kulingana na wote Yesu na Maandiko, Mungu ametupa sheria ya maadili kuitii. Na si tu tumegeuza migongo yetu kwa uhusiano pamoja naye, pia tumevunja sheria hizi za maadili kwamba Mungu ameziweka. Wengi wetu twajua baadhi ya Amri Kumi za Mungu:
“Usiseme uongo, usiimbe, usiue, usizini,” etc. Yesu aliweka kwa ufupi kwa kusema tumpende Mungu kwa moyo wetu wote na jirani zetu kama sisi wenyewe tunavyojipenda. Dhambi, kwa hiyo si tu mbaya tuifanyao katika kuvunja sheria, lakini pia kushindwa kwetu kufanya mema yaliyo sahihi.
Mungu aliumba ulimwengu pamoja na sheria ambazo zinaongoza kila kitu ndani yake. Hazivunjwi na wala hazibadilishiki. Wakati Einstein alipokokotoa fomyula E=MC2, alivumbua siri ya nguvu za nyukilia. Kuweka michanganyiko sahihi pamoja katika mazingira yahitajiyo nguvu na nguvu kubwa inapatikana. Maandiko yanatuambia kwamba sheria ya maadili ya Mungu ni muhimu kwa sababu inatokana na tabia yake.
Tangu mwanamme na mwanamke wa mwanzo, hatukutii sheria la Mungu, ingawaje ni nzuri kwa ajili yetu. Na tumeshindwa kufanya yaliyo sahihi. Tumerithi hali hii tangu mtu wa kwanza, Adam. Biblia inaita kutotii huku, dhambi, ambayo inamaanisha “kukosa shabaha” kama mwindaji anavyokosa shabaha yake aliyokusudia. Hivyo, dhambi zetu zimevunja uhusiano wa Mungu aliokusudia pamoja na sisi. Tukitumia mfano wa mwindaji, tumekosa shabaha linapokuja suala la madhumuni tuliyoumbiwa kwayo.
Dhambi inasababisha kusitisha mahusiano yote: maisha ya mwanadamu yalikoma katika mazingira yake (kutengwa), kila mmoja alijitenga mbali wengine (kukosa na aibu), watu walijitenga na watu wengine (vita, mauaji), na watu walijitenga na Mungu (kifo cha kiroho). Kama viungio katika mnyonyoro, mara kiungio cha kwanza kati ya Mungu na ubinadamu vilipovunjika, mkusanyiko wa viungio vyote vikawa vimejitenga.
Na tumekatishwa. Kama Kanye West anavyorapu, “Na sifikiri kuna kitu chochote ninachoweza kufanya kuyapendezesha makosa yangu. Ninataka kuzungumza kwa Mungu lakini ninaogopa hatujaongea naye muda mrefu….” Mashairi ya nchi za magharibi yanazungumzia utengano ambao dhambi inaleta katika maisha yao. Na kulingana na Biblia, utengano huu ni zaidi ya ushairi katika wimbo wa kurapu/kufoka. Una matokeo ya hatari zaidi.
Dhambi zetu zimetutenga na upendo wa Mungu
Uasi wetu (dhambi) umetengeneza ukuta wa utendano kati ya Mungu na sisi (Angalia Isaya 59:2). Katika Maandiko, “Kutengwa” kunamaanisha kifo cha kiroho.. Na kifo cha kiroho kinamaanisha kutengwa kabisa kutoka katika nuru na maisha ya Mungu.“Lakini subiri dakika moja,” unaweza kusema “Mungu hakujua yote ya hayo kabla hajatuumba?
Kwanini hakuona mpango wake ulilaumiwa kwa kushindwa?” Bila shaka Mungu ajuaye yote angetambua kwamba tungeasi na kutenda dhambi. Kwa kweli, ni kushindwa kwetu ambako kunafanya mpango wake uchanganye sana akili. Hii inatufanya tufikie sababu kwamba Mungu alikuja dunia katika umbile la mwanadamu Na hata kwa kushangaza-—sababu yake kuu isiyo ya kawaida ya kifo chake.
Ufumbuzi kamili wa Mungu
Wakati wa miaka yake mitatu ya idara ya hadhara. Yesu alitufundisha jinsi gani kuishi na kufanya miujiza mingi, hata kufufua wafu. Lakini alisema kwamba mpango wake wa msingi ni kutuokoa kutoka katika dhambi zetu.Yesu alitangaza rasmi kwamba alikuwa Masiha ambaye angechukua uovu wetu juu yake. Nabii Isaya aliandika kuhusu Masiha miaka 700 mapema kabla, akitupa sisi siri chache kuhusu wasifu wake. Lakini siri ngumu zaidi ni kwamba Masiha angekuwa wote mtu na Mungu!
“Kwetu sisi, mtoto amezaliwa, kwetu sisi mtoto ametolewa. Na jina lake ataitwa Mwenyezi Mungu, Baba wa milele, Mtoto-Mfalme wa Amani” (Isaya 9:6).
Mtunzi Ray Stedman anaandika Masiha aliyeahidiwa wa Mungu: Tangu mwanzo kabisa wa Agano la Kale, kuna ishara ya matumaini na matarajio, kama sauti ya nyayo zikaribiazo: Mtu fulani anakuja… matumaini hayo yanaongezeka katika rekodi yote ya kinabii kama nabii baada ya nabii atangazapo kidokezo kingine kinachotamanisha: fulani anakuja!”[8]
Manabii wa kale walikwishatabiri kwamba Masiha angekuwa sadaka ya dhambi kamilifu ya Mungu, akitimiliza haki yake. Huyu mtu mkamilifu angefaulu kufa kwa ajili yetu. (Isaya 53:6).
Kulingana na waandishi wa Agano Jipya, sababu ya pekee Yesu alifaulu kufa kwa ajili ya sisi wengine ni kwa sababu kama Mungu, aliishi maisha kamilifu ya kimaadili na hakuwa mlengwa kwa hukumu ya dhambi.
Ni vigumu kuelewa jinsi gani kifo cha Yesu kililipia dhambi zetu. Labda mijadala ya kisheria ingeweza kubainisha namna gani Yesu anatatua mkanganyiko kuhusu upendo kamili wa Mungu na haki.
Fikiria unaingia chumba cha mahakama, una hatia ya mauaji (una baadhi ya masuala nyeti). Unapokaribia benchi, unatambua kwamba jaji ni baba yako. Huku ukijua kwamba anakupenda, unaanza kujitetea kwa haraka, “Baba, niache niende”.
Kwayo anajibu, “Nakupenda, kijana, lakini mimi ni jaji. Siwezi kukuacha uende kirahisi.”
Anagawanyika/anakuwa na uamuzi mgumu. Mwisho anagonga kifimbo chake na anakutangaza wewe ni mwenye hatia. Haki haiwezi kulegezwa, kwa vovyote vile hata na jaji. Lakini kwa sababu anakupenda, anatelemka kutoka katika kiti, anaondoa kamba, na anajitoa kulipa adhabu kwa ajili yako. Na kwa kweli, anakaa sehemu ile badala yako katika kiti cha umeme.
Hii ni picha iliyochorwa na Agano Jipya. Mungu alishuka katika historia ya mwanadamu, katika nafsi ya Yesu Kristo, na akaenda katika kiti cha umeme (soma: msalaba) badala yetu sisi kwa ajili yetu. Yesu si kijakazi wa upande baki, anayechukua dhambi zetu, bali ni Mungu yeye mwenyewe. Tunaweza kusema, Mungu na chaguzi mbili: kuhukumu dhambi ndani yetu au kuchukua adhabu mwenyewe. Kwa Kristo, alichagua chaguo la mbili.
Ingawaje U2′s Bono hajifanyi kuwa mwanateolojia, kwa usahihi anaeleza sababu ya Kifo cha Yesu:
“Hoja ya kifo cha Kristo ni kwamba Kristo alichukua dhambi za duni, ili kile tulichokiondoa kisirudi tena kwetu, na kwamba asili yetu ya dhambi isivune kifo dhahiri. Hiyo ni pointi. Inafaa itufanye tuwe wanyenyekevu. Si tu kazi nzuri zetu wenyewe ambazo zinatupeleka katika mageti ya Mbinguni.”[9]
Na Yesu aliiweka wazi kwamba ni yeye pekee anayeweza kutupeleka sisi kwa Mungu, akisema “Mimi ni njia, ukweli na uzima”. “Hakuna anayekuja kwa Baba isipokuwa kupitia kwangu.” (Yohana 14:6)
Lakini wengi wamebisha kwamba dai la Yesu kwamba yeye ni njia ya pekee kwa Mungu ni jembamba, wanasema kuna njia nyingi kwenda kwa Mungu. Hao wanaoamini dini zote ni sawa wanakana tuna tatizo la dhambi. Wanakataa kuchukua maneno ya Kristo kihakika. Wanasema upendo wa Mungu utatukubali sisi sote bila kujali tulichofanya.
Labda Hitler anastahili adhabu,
wanatoa sababu, lakini sio wao au wengine wanaoishi “maisha ya heshima”. Ni
kama kusema kwamba Mungu anaweka gredi kwa mstari, na kila mtu anayepata D au
zaidi ataingia ndani. Lakini hili linaleta mkanganyiko.
Kama tulivyoona, dhambi ni kinyume
kabisa cha tabia takatifu ya Mungu. Hivyo tumemkosea yule aliyetuumba, na
aliyetupenda kiasi cha kutosha kumtoa sadaka mwanawe kwa ajili yetu. Katika
maana ya uasi wetu ni kama kutema kwenye uso wake. Wala si matendo mazuri,
dini, kufikiria, au Karma kunaweza lipa deni dhambi zetu zilizoingia.
Kulingana na mwanateolojia R.C
Sproul, Yesu pekee ndiye anayeweza lipa deni hilo. Anaandika:
“Musa aliweza kupatanisha katika
sheria; Muhammad aliweza kutumia upanga; Buddha aliweza kutoa ushauri binafsi;
Confucius aliweza kutoa misemo ya busara; lakini hakuna mmoja kati ya hawa watu
alifaulu kutoa malipo kwa dhambi za dunia…. Kristo pekee ni mwenye thamani kwa
kujitoa kusiko na kikomo na huduma.”[10]
Zawadi
isiyo stahiki
Neno
la kibiblia kuelezea msamaha wa bure wa Mungu kupitia kifo cha kujitoa sadaka
cha Yesu ni rehema. Wakati huruma inatuokoa kutoka katika kile tunachostahili,
rehema ya Mungu inatupa sisi kile ambacho hatustahili. Hebu turejee kwa dakika
jinsi gani Kristo alivyotendea kile tusingeweza kufanya kwa ajili yetu:
- Mungu alitupenda na alituumba kwa ajili ya uhusiano na Yeye.[11]
- Tumepewa uhuru kukubali au kukataa uhusiano huo.[12]
- Dhambi zetu na uasi dhidi ya Mungu na sheria zake umetengeneza ukuta wa utendano kati yetu na Yeye Mungu.[13]
- Ingawa tunastahili hukumu ya milele, Mungu amelipa deni letu kwa ukamilifu kwa Kifo cha Yesu kwetu, kufanya uzima wa milele pamoja na Yeye uwezeke.[14]
Bono anatupa mtazamo wake kwenye
rehema.
“Rehema inabatilisha sababu na maana
Upendo inaingilia kati, ukipenda, matokeo ya matendo yako, ambao kwa mazingira
yangu ni habari nzuri sana kwa sababu nimefanya mambo mengi ya kipambavu….
Ningekuwa katika matatizo makubwa iwapo Karma angekuja kunihukumu mwishowe….
Haisahaulishi makosa yangu, lakini ninaepushwa kwa rehema.
Ninaepushwa/nisamehewa kwamba Yesu alichukua dhambi zangu kwenye msalaba, kwa
sababu ninajua mimi ni nani, na ninatumai sihitaji kutegemea dini yangu
mwenyewe.”[15]
Sasa tuna picha ya mpango wa Mungu
wa muda mrefu ikijiweka pamoja. Lakini kuna kitu kimoja kinakosekana. Kulingana
na Yesu na waandishi wa Agano Jipya, kila mmoja wetu pekee lazima aitikie na
apokee zawadi ya bure Yesu anayotupatia sisi. Hatatulazimisha kuipokea.
Unachagua hatima
Tunaendelea kufanya chaguo—kitu gani cha kuvaa, kitu gani cha kula, fani zetu, mwenzi wa ndoa, n.k. Ni sawa sawa wakati inapohusu uhusiano na Mungu. Mwandishi Ravi Zacharias anaandika:
“Ujumbe wa Yesu unadhihirisha kwamba kila mmoja… anakuja kumjua Mungu si kwa sababu ya kuzaliwa kwake, lakini kwa chaguo hai ili kumruhusu Yeye Mungu awe na taratibu katika maisha yake.”[16]Chaguo zetu mara nyingi zinaathiriwa na wengine. Lakini katika mazingira fulani tunapatiwa ushauri mbaya. Tarehe 11 Septemba, 2001, watu wasio na hatia 600, waliweka imani yao katika ushauri potofu, na bila hatia walihangaikia matokeo yake. Hadithi ya kweli inaendelea kama hivi:
Mtu mmoja ambaye alikuwa katika sakafu/ghorofa ya 92 ya jengo ka kusini la Kituo cha Biashara Duniani (WTC) alikwishasikia mpasuko katika jengo la kaskazini. Akishangazwa na mlipuko, aliwaita Police kwa ajili ya maelekezo kuhusu ni afanye. “Tunahitaji kujua ikiwa tunahitaji kutoka hapa, kwa sababu tunajua kuna mlipuko,” alisema kwa kwa haraka mara moja kwenye simu.
Sauti katika upande mwingine ulimshauri asitoke. “Nitasubiri hadi nipate taarifa zaidi.”
“Yote sawa” msemaji alisema. “Usitoke.” Kisha akakata/akatundika simu.
Muda mfupi baada ya saa 3:00 asubuhi, ndege nyingine ikajikita katika sakafu ya 80 ya jengo la kusini. Karibia watu wote 600 katika sakafu za juu za jengo-mnara la kusini waliangamia. Kushindwa kutoka katika jengo kulikuwa ni mojawapo ya misiba mikubwa ya siku hiyo.[17]
Watu hao 600 waliangamia kwa sababu walitegemea taarifa zisizo sahihi ingawaje zilitolewa na mtu ambaye alikuwa akijaribu kusaidia. Msiba usingetokea ikiwa waathirika 600 wangekuwa wamepewa taarifa sahihi.
Chaguo letu hai kuhusu Yesu ni muhimu zaidi kuliko lile moja lililowakabili waathirika waliotaarifiwa vibaya wa Septemba 11. Kuishi milele kuko mashakani. Tunaweza kuchagua moja kati ya miitikio mitatu. Tunaweza kumdharau. Tunaweza kumkataa. Au, tunaweza kumkubali.
Sababu kubwa watu wengi wanapitia katika maisha wakimdharau Mungu ni kwamba wako kazini sana wakilazimisha agenda zao. Chuck Colson alikuwa kama hao. Katika umri wa miaka 39, Colson alichukua ofisi karibu na Raisi wa Marekani. Alikuwa ni “kijana shupavu” wa ikulu ya Nixon, “mtu wa maamuzi magumu” ambaye angeweza kufanya maamuzi magumu. Lakini kashifa ya Watergate iliharibu sifa yake na maisha yake yakawa hayana mwelekeo. Baadaye akaandika:
“Nimekuwa nikijijali nafsi yangu. Nimefanya hili na hilo, nimefaulu, nimefanikiwa na sijampa Mungu heshima yoyote, hata mara moja sijamshukuru kwa zawadi zake kwangu. Sijafikiria kitu chochote kuwa kikubwa sana kwangu, au hata kama katika nyakati fupi nilifikiria kuhusu mamlaka makubwa ya Mungu, sijamhusianisha Yeye na maisha yangu.”[18]
Wengi wanaweza kutambua hilo pamoja na Colson. Ni rahisi kukamatwa katika hatua za haraka za maisha na kuwa na muda kidogo au hakuna muda kwa ajili ya Mungu. Lakini bado kudharau zawadi ya rehema za Mungu ya msamaha una matokeo makubwa sawa na kukataa moja kwa moja. Deni letu la dhambi lingebaki bado bila kulipwa.
Katika kesi za jinai, wachache wamekataa msamaha. Mwaka 1915 George Burdick, mhariri jijini wa Gazeti la Baraza la New York, alikataa kudhihirisha vyanzo na sheria zinazovunjwa. Raisi Woodrow Wilson alitangaza msamaha wote kwa Burdick kwa makosa “yaliyokwishafanya na yale huenda alifanya” Kitu kilichofanya kesi ya Burdick iwe kihistoria ni kwamba alikataa msamaha. Hiyo ilileta kesi kwenye Mahakama Kuu, ambayo iliungana na Burdick ikisema kwamba msamaha wa Raisi usingelazimishwa kwa kila mtu.
Linapokuja suala la kukataa msamaha kamili wa Kristo, watu wanatoa aina-tofauti za sababu. Wengi wanasema hakuna ushahidi wa kutosha, lakini, kama Bertrand Rusell na kundi la wakosozi wengi, hawavutiwi vya kutosha kuchunguza hasa. Wengine wanakataa kuangalia mbele zaidi ya wakristo wanafiki wanaowajua, wakilaumu tabia zisizobadilika na zisizopendeza kama kisingizio. Na wengine bado wanamkataa Kristo kwa sababu wanamlaumu Mungu kwa matukio ya huzuni na kusikitisha waliyohangaikia.
Hata hivyo Zacharia, aliyejadiliana na wenye akili kwenye mamia ya maeneo ya vyuo anaamini kwamba sababu ya kweli ambayo watu wanamkataa Mungu ni ya kimaadili. Anaandika:
“Binadamu hamkatai Mungu kwa sababu ya mahitaji ya kiakili wala kwa uchache wa ushuhuda. Mwanadamu anamkataa Mungu kwa sababu ya ubishi wa kimaadili ambao unakataa kukubali kumhitaji kwake Mungu.”[19]
Tamaa kwa ajili ya uhuru wa kimaadili ulimweka C.S Lewis mbali na Mungu kwa sehemu kubwa ya miaka yake ya chuoni. Baada ya kutafuta kwake ukweli, kulimwongoza kwa Mungu, Lewis anaeleza jinsi gani kumkubali Kristo kulihusisha zaidi ya makubaliano ya werevu wa ukweli. Anaandika:
“Mwanadamu aangukaye si tu kiumbe asiye mkamilifu anayehitaji kustawi: ni muasi ambaye lazima alaze chini mikono yake. Kulaza chini mikono yako, kusalimu amri, kusema unasikitika, kutambua kwamba umekuwa kwenye njia potofu na unakuwa tayari kuanza maisha upya tena ndiyo kile wakristu wanaita kutubu.”[20]
Kutubu ni neno ambalo linamaanisha mkengeuko mkubwa katika kufikiri. Hicho ndicho kile kilichotokea kwa Nixon “msuluhishi wa zamani”. Baada ya Kashifa ya Watergate kuwekwa wazi, Colson alianza kufikiria kuhusu maisha kitofauti. Akitambua kukosa kwake mwenyewe kwa kusudio, alianza kusoma Ukristu wa Lewis, uliopewa kwake na rafiki. Akiwa amefundishwa kama mwanasheria, Colson alichukua muhuri wa njano na alianza kuandika mahojiano ya Lewis. Colson alikumbuka:
“Nilijua wakati ulikuwa umefika kwangu…. Nilipaswa kukubali bila majadiliano Yesu Kristo ni Bwana wa maisha yangu? Ni kama geti mbele yangu. Kulikuwa hakuna njia kulikwepa. Nilipaswa kuliingia kulipita au ningebaki nje. Labda au nahitaji muda zaidi nilikuwa najidanganya mwenyewe.”
Baada ya mabadilishano ya fikra ya ndani, huyu msaidizi kwa raisi wa Marekani, mwishowe alitambua kwamba Yesu Kristo alikuwa anastahili uaminifu wake wote. Anaandika:
“Na mapema asubuhi Ijumaa wakati nimekaa peke yangu nikikodolea macho bahari niipendayo, maneno ambayo sikuwa na uhakika nayo, niliweza kuelewa au kusema au yalitoka yenyewe mdomoni mwangu.’Bwana Yesu, ninakuamini. Ninakukubali wewe. Tafadhali njoo katika maisha yangu. Ninaamua maisha yangu yawe kwako.’”[21]
Colson aligundua kwamba maswali
yake, “Mimi ni nani?” “Kwani nipo hapa?” na “Wapi ninaenda?” yote yanajibiwa
katika uhusiano pekee na Yesu Kristo. Mtume Paul anaandika, “Ni katika Kristo
ambamo tunajua sisi ni nani na kitu gani tunaishi kwacho.” (Waefeso 1:11,
Ujumbe).
Tunapoingia katika uhusiano binafsi
na Yesu Kristo, anajaza pengo letu la ndani, anatupa amani, na anaridhisha hamu
zetu za maana na matumaini. Na hatuhitaji kujiweka katika vichocheo vya muda
kwa ajili ya kutimiliza kwetu. Anapoingia kwetu sisi, pia anatimiza matamanio
yetu ya ndani na mahitaji kwa ajili ya usalama wa kweli na upendo unaodumu.
Na kitu cha kushangaza ni kwamba
Mungu mwenyewe alikuja kama mwanadamu kulipa deni letu lote. Kwa hiyo, hatuko
tena katika adhabu ya dhambi. Paulo anasema hili waziwazi kwa warumi pale
anapoandika,
“Mlikuwa maadui wake mliotengwa
kutoka kwake kwa mawazo na matendo yenu maovu, lakini sasa amewarejesha kama
rafiki zake. Amefanya hili kupitia kifo chake msalabani katika mwili wake
mwenyewe wa kibinadamu. Matokeo yake, amewaleta katika uwapo wa Mungu, ninyi ni
watakatifu na bila lawama mkisimama mbele yake bila kosa hata moja””(Wakolosai
1:21b-22a NLT).
Hivyo Mungu alifanya kile hatukuweza
kufanya kwa nafsi zetu. Tumewekwa huru kutoka katika dhambi zetu kwa kifo
kitakatifu cha Yesu. Ni kama muuaji wa halaiki anayepelekwa mbele ya jaji na
anapewa msamaha wote. Hastahili msamaha, wala sisi pia hatustahili msamaha.
Zawadi ya Mungu ya uzima wa milele ipo bure kabisa – na ipo tayari kwa ajili ya
kuchukua. Lakini ingawaje msamaha unatolewa kwetu, ni juu yetu kuukubali.
Chaguo ni lako.
Upo katika mahali katika maisha yako
ambapo ungependa kuikubali ofa ya bure ya Mungu?
Labda kama Madonna, Bono, Lewis na
Colson, maisha yako yamekuwa bure kabisa. Hakuna kitu ulichojaribu kimeridhisha
kiu ya ndani unayosikia. Mungu anaweza kuridhisha kiu hiyo na kukubadili katika
muda mfupi. Alikuumba uwe na uhai ambao umejazwa na maana na makusudio. Yesu
alisema, Dhumuni langu ni kutoa uzima katika ukamilifu wake wote.” (Yohana
10:10b)
Au labda mambo yanaenda vizuri kwako
katika maisha lakini haujatulia na umekosa amani. Unatambua kwamba umevunja
sheria za Mungu na umetengwa kutoka katika upendo na msamaha wake. Unahofia
hukumu ya Mungu Yesu alisema, “Ninawaachia zawadi — amani ya akilini na moyoni.
Na amani ninayotoa si kama amani dunia itoayo.”
Hivyo iwe kwamba umechoshwa na
maisha ya ufuatiliaji bure au unasumbuliwa na kukosa amani kwa Muumbaji wako,
jibu lipo katika Yesu Kristo.
Unapoweka imani yako katika Yesu
Kristo, Mungu atakusamehe dhambi zako zote, za zamani, sasa na wakati ujao na
kukufanya wewe mtoto wake. Na ukiwa kama mtoto wake akupendaye, anakupa wewe
dhumuni na maana katika maisha duniani na anaahidi uzima wa milele pamoja naye.
Maneno ya Mungu yanasema, “kwa wote
waliomwamini na kumkubali, aliwapa haki ya kuwa watoto wa Mungu.” (Yohana 1:12)
Msahama wa dhambi, makusudio katika
maisha, na uzima wa milele yote ni yako kuuliza. Unaweza kumualika Kristo
katika maisha yako sasa hivi kwa imani kupitia maombi. Maombi/Sala ni kuongea
na Mungu. Mungu anajua moyo wako hahusiki kama maneno yako kwa sababu yupo
pamoja na msimamo wa moyo wako. Ifuatayo ni sala iliyopendekezwa:
“Mpendwa Mungu, ninataka kukujua
wewe binafsi na kuishi milele pamoja na wewe. Nakushukuru wewe, Bwana Yesu kwa
kufa msalabani kwa dhambi zangu.. Nafungua mlango wa maisha yangu na kukupokea
wewe kama mkombozi na Bwana. Ongoza maisha yangu na nibadili mimi, nifanye mimi
aina ya mtu unayetaka niwe.”
Maombi haya yanaeleza hitaji la moyo
wako? Ikiwa ni hivyo, sali maombi yaliyopendekezwa hapo juu kwa lugha yako ya
asili.
Mara Chuck Colson alipotoa maisha
yake kwa Kristo, mtu huyu ambaye alishamtumikia Raisi wa Marekani, sasa
alifurahi katika kumtumikia Mungu wa ulimwengu. Alianza kuwasaidia wengine
kugundua uhuru na furaha aliyogundua katika Kristo.
Baada ya kutumikia muda gerezani kwa
makosa yake ya kashifa ya Watergate, Mungu alimpa Colson upendo mpya na kujali
kwa ajili ya wafungwa. Kujali kwake kupya kwa hao waliokwamisha jamii
kulimfanya kuanzisha Ushirika wa Magereza,” idara ambayo imeshirikiana kujua
ukweli na rehema za Yesu Kristo kwa mamilioni ya wafungwa duniani kote.
Yesu pia amefanya imewezekana kwako
kupata maisha ya maana, madhumuni na nguvu. Anakupenda wewe na ana mpango wa
kupendeza kwa ajili ya maisha yako ambao unaweza kuanza upya leo, bila kujali kushindwa
kwako kwa zamani na dhambi.
Kiunganishi hapa chini kinatoka
taarifa bure ambazo zitakusaidia wewe kugundua ahadi za msingi za kibiblia
kuhusiana na safari yako pamoja na Kristo.
Je
ni kweli Yesu alifufuka toka katika Wafu?
Mashahidi wa macho kwa Yesu Kristo
kwa kweli walizungumza na walitenda kama walivyoamini, walimwabudu kama “Bwana”
lakini lazima tuuchukue ufufuko wa Yesu Kristo kwa imani pekee, au kuna
ushahidi mzito wa kihistoria?. Wakosoaji wachache walianza uchunguzi kwenye
rekodi za kihistoria kuthibitisha maelezo ya ufufuko ni uongo. Ni kitu gani
waligundua?
Kulikuwa
na Hila za Da Vinci ?
Kulikuwa na Hila za Da Vinci ambazo
zilibadilisha historia ya kweli ya ukristu? Je Constantine aliagiza uharibifu
wa rekodi za kweli za Yesu Kristo akatuachia historia ya uongo ya Yesu Kristo
na mitume?
“Kulikuwa na hila za Da Vinci,”
inachunguza dhana za hila za dunia zinaoongoza kuhusu Yesu Kristo, ikijibu
madai yake kwa ushahidi.
Unapoamua kujitoa kwa Yesu Kristo,
anaingia katika maisha yako, anakuwa mwongozo wako, mshauri wako, mfariji wako,
na rafiki yako bora zaidi. Zaidi ya hapo, anakupa wewe nguvu kushinda majaribu,
vishawishi, anakuweka huru kukabili maisha mapya yaliyojaa maana, madhumuni na
nguvu.
Chuck Colson aligundua madhumuni
mapya na nguvu. Colson anakiri kwamba kabla ya kuwa mkristu, alikuwa mwenye
tamaa, majivuno na mbinafsi. Alikuwa hana haja wala hamu ya kuwapenda wengine
wanaohitaji. Lakini mawazo yake na motisha zake kwa kiasi kikubwa zilibadilika
mara alipojitoa kwa Kristo.
No comments:
Post a Comment