Yesu na Maria Magdalena: Walikuwa na ndoa ya siri?
Injili
ya Maria (Magdalena)
Wazo kwamba Maria Magdalena alikuwa
mtu maalum kwa Yesu inachukuliwa hasa kutoka Injili ya Maria. Injili hii ya
Kinostiki (Kijuaji) si sehemu ya Agano Jipya, na iliandikwa na mtunzi
asiyejulikana katika nusu ya karne ya pili, au karibia miaka mia na hamsini
baada ya kifo cha Yesu. Hakuna mashahidi wa macho, akiwamo Maria mwenyewe
wangekuwa hai wakati ilipoandikwa (karibia miaka 150 A. D.). Tarehe hiyo ya
mwishoni inamaanisha Injili ya Maria haikuandikwa na shahidi wa macho wa Yesu,
na hakuna anayejua aliyeiandika.
Aya moja katika Injili ya Maria
inamwelezea Maria Magdalena kama mfuasi kipenzi wa Yesu, inasema alimpenda
Maria zaidi kuliko sisi (maana yake wafuasi wake)” Katika aya nyingine Peter
inavyoaminika alimwambia Maria, Dada, twajua mwokozi alikupenda zaidi ya
mwanamke mwingine yeyote” Lakini hakuna kilichoandikwa katika Injili ya Maria
kinachozungumzia mapenzi au uhusiano wa kimapenzi kati ya Maria Magdalena na
Yesu.
Injili
ya Philipo
Maandiko ya Da Vinci yameweka dai lake kwamba Yesu na Maria walikuwa wameoana na
walikuwa na mtoto kwenye aya moja pekee katika Injili ya Kinostiki (Kijuaji) ya
Philipo ambayo inaonesha Yesu na Maria walikuwa marafiki. Aya hii inasema:
(Mabano yanaonekana ambapo maneno ya andiko yanakosekana au hayasomeki)
“Wanawake watatu siku zote
walitembea na BWANA: Maria mama yake, dada na Maria Magdala ambaye aliitwa
mwenzi wake. Kwa “Maria” ni jina la dada yake, mama yake na mwenzi/rafiki wake”
In mtaalamu wa Maandiko ya kubuni
ya Da Vinci, Sir Leigh Teabing anasema kwamba neno kwa neno rafiki
lingeweza kumaanisha mwenzi. Lakini kulingana na wasomi, hiyo ni tafsiri
isiyoelekea. Kwa kuanza, neno kwa ujumla lililotumika kwa mke katika Agano Jipya
Kigiriki ni “gune” sio “koinonos” Ben Witherington III, akiandika katika Rejea
ya Kibiblia ya Elimu-Kale, alizungumzia pointi hii muhimu:
“Kulikuwa na neno lingine la
Kigiriki, gune, ambalo lingeweka neno hili wazi. Ni kama neno koinonos
hapa linamaanisha “dada” katika maana ya kiroho kwa sababu hivyo ndivyo
linavyotumika mahali pengine pote katika aina hii ya uandishi. Katika hali
yoyote, maandishi haya hayasemi waziwazi wala kudokeza kwamba Yesu alikuwa
amemuoa Maria Magdalena.”[1]
Kuna aya moja pia katika Injili ya
Philipo ambayo inasema Yesu alimbusu Maria.
“Mwenzi ni Maria wa Magdala. Alim…
yeye zaidi ya wafuasi, alimbusu yeye mara nyingi kwenye. Mwingine …alimwambia,
‘Kwanini unampenda yeye zaidi kuliko sisi sote?’”
Kuwasalimia marafiki kwa busu
kulikuwa kawaida katika karne ya kwanza, na hakukuwa na ishara ya mapenzi.
Profesa Karen King anaeleza kwenye kitabu chake Injili ya Maria Magdala, kwamba
busu katika maandiko ya Philipo hasa ilikuwa ni busu safi lisilo la mapenzi
bali la ushirika/umoja.
Lakini labda muhimu zaidi ni ukweli
kwamba Injili ya Philipo iliandikwa na mtunzi asiyejulikana karibu miaka 200
baada ya maelezo ya mashahidi wa macho wa Agano Jipya (Angalia saa Andiko la Yesu
na saa Tabasamu la MonaLisa.
Ni muhimu pia kufahamu kwamba, mbali
ya hivi vifungu vichache kwa kuulizwa, hakuna andiko lingine la kihistoria
ambalo linadokeza Yesu na Maria walikuwa na uhusiano wa kimapenzi. Hakuna
mwanahistoria wa kawaida, au mwanahistoria wa kikristu aliyeandika hata robo kuhusu
uhusiano huo. Na kwa sababu Injili zote, Injili ya Maria na Injili ya Philipo
ziliandikwa miaka 100 – 220 baada ya Kristo na watunzi wasiojulikana, maelezo
yao kuhusu Yesu na Maria yanahitaji kutathminiwa katika mazingira yote ya
historia ya wakati ule na maandiko ya mwanzoni kabisa ya Agano Jipya.
Yesu na Maria Magdalena: Walikuwa na ndoa ya siri?
Uamuzi
wa Wasomi
Lakini je, kanisa la kale lingeweza
kuharibu ushahidi katika jaribio lao la kuandika upya historia ya Yesu? Bila
shaka hicho ndicho kitu Jacobovici, Brown, na kundi la wapiga chuku yaani
waandika vioja au wadadisi wengine wanachosema. Lakini wasomi wanakubaliana
nacho?
Makala ya gazeti la Newsweek inaandika kwa kifupi maoni ya wasomi yanayoongoza, kwa
uwazi yakisema kwamba wazo la Yesu na Maria Magdalena walioana hayana msingi wa
kihistoria.[2] Labda
wanostiki yaani wazushi wajuaji wachache walifikiri Agano Jipya lilikuwa na
aibu kuhusiana na mapenzi na wakaamua kulikoleza suala hilo kidogo. Kwa sababu
yoyote ile, aya hizi zilizotengwa na zilizojificha ziliandikwa miaka 100 – 200
baada ya Kristo haziko zaidi katika kuikita nadharia ya hila za njama juu yake.
Usomaji wa kuvutia labda, lakini kabisa siyo historia.
Lakini baadhi wanabaki hawaamini.
Labda wanataka tu kuifanya historia ivutie zaidi. Mwandishi wa habari za
televisheni aliyeshinda tuzo Frank Sesno aliuliza jopo la wasomi wa kihistoria
kuhusu tabia ya kuvutiwa na kitu watu waliyo nayo kwa nadharia ya hila za
njama. Profesa Stanley Kutler kutoka Chuo Kikuu cha Wisconsin alijibu, “Wote
tunapenda matukio ya ajabu ya siri, lakini tunapenda habari za njama zaidi.”[3]
Labda habari zote kuhusu Yesu na
Maria zina umuhimu zaidi wa kufanya kwa wapinzani wa ukristu wakijaribu
kumfanya aonekane binadamu wa kawaida mtu ambaye wakristu tangu mwanzo
wamemwita “Mungu” (Kusoma zaidi kuhusu jinsi gani wakristu wa zamani walimwona
Yesu (Angalia saa Tabasamu la MonaLisa).
Kwa mfano, mtume Paulo alisema kuhusu Yesu Kristo:
“Ingawa alikuwa Mungu, hakuhitaji na
kushikilia hadhi zake kama Mungu. Alijifanya hana kitu, alichukua nafasi ya unyenyekevu
ya mtumwa na alionekana katika umbo la kibinadamu” (Wafilipi 2:6, 7a).
Yohana, shahidi wa macho, na mmoja
wa wafuasi wa karibu wa Yesu, alimzungumzia hivyo.
“Katika mwanzo neno tayari
lilikuwapo. Alikuwa pamoja na Mungu, na alikuwa Mungu… aliumba kila kitu
kilichopo… hivyo neno likawa mwanadamu na likaishi hapa duniani miongoni
mwetu.”(sehemu za Yohana 1:1-3, 14).
Je
ni kweli Yesu alifufuka toka katika Wafu?
Swali kubwa kabisa la wakati wetu si
kwamba Yesu na Maria Magdalena walioana, lakini “Nani ni Yesu Kristo wa Kweli?”
Alikuwa mtu wa kipekee, au alikuwa Mungu katika mwili, kama Paulo, Yohana, na
wafuasi wake wengine walivyoamini?
Mashahidi wa macho kwa Yesu Kristo
kwa kweli walizungumza na walitenda kama walivyoamini, aliinuka kimwili toka
katika wafu baada ya kusulubiwa kwake. Ikiwa hawakuwa sahihi basi Ukristu
umejengwa katika uongo. Lakini kama walikuwa sahihi, muujiza huo ungethibitisha
yote Yesu alisema kuhusu Mungu, yeye mwenyewe na sisi.
Lakini lazima tuchukue ufufuko wa
Yesu Kristo kwa imani pekee, au kuna ushahidi mzito wa kihistoria? Wakosoaji
wachache walianza uchunguzi kwenye rekodi za kihistoria kuthibitisha maelezo ya
ufufuko ni uongo. Ni kitu gani waligundua? Saa Yesu Alifufuka Wafu.
Kulikuwa
na Hila za Da Vinci ?
“Tabasamu la Monalisa” inachunguza
fikra kuhusu njama zinaoongoza duniani kuhusu Yesu Kristo. Je, Yesu na Maria
Magdalena waliooana? Je Constantine aliagiza uharibifu wa rekodi za kweli za Yesu
Kristo akimwelezea upya kuwa Mungu wakristu wanavyomwabudu leo? Saa Tabasamu la MonaLisa.
Je,
Yesu alisema kitu gani kinatokea baada ya sisi kufa?
Ikiwa ni kweli Yesu alifufuka toka
katika Wafu, basi lazima ajue kitu gani kipo upande mwingine. Ni kitu gani
alisema kuhusu maana ya maisha na siku zetu zijazo? Kuna njia nyingi kwenda kwa
Mungu au Yesu alidai kuwa njia pekee? Soma majibu ya kushangaza “Kwanini Yesu?”
Saa Kwanini Yesu?
Je,
Yesu anaweza kuleta maana katika maisha?
“Kwanini Yesu? inaangalia suala la
kwamba Yesu ni muhimu leo. Je, Yesu anaweza kujibu swali kubwa la maisha: “Mimi
ni nani?” “Kwanini niko hapa?” na, “Wapi ninaenda?” Makanisa yaliyokufa na
misalaba imewaongoza wengine kuamini kwamba hawezi, na kwamba Yesu ametuacha
sisi kuendana na dunia iliyo nje isiyo na udhibiti. Lakini Yesu amefanya madai
kuhusu maisha na madhumuni yetu hapa duniani ambayo yanahitaji kuchunguzwa
kabla hatujamkataa kama asiyejali na asiye na nguvu. Makala hii inachunguza
siri ya kwanini Yesu alikuja duniani. Saa www.Kwanini Yesu?
Ni
kweli Yesu alifufuka toka katika Wafu?
Mashahidi wa macho kwa Yesu Kristo
kwa kweli walizungumza na walitenda kama walivyoamini, alifufuka toka katika
wafu baada ya kusulubiwa kwake. Ikiwa walikosea basi uKristu umeanzishwa kwa
uongo? Lakini kama walikuwa sahihi, muujiza huo ungethibitisha yote Yesu
aliyosema kuhusu Mungu, kuhusu yeye na kutuhusu sisi.
Lakini ni lazima tuamini ufufuko wa
Yesu Kristo kwa imani pekee, au kuna ushahidi wowote wa kihistoria? Wakosoaji
kadhaa walianza uchunguzi kwenye kumbukumbu za kihistoria kujaribu kuona kama
kweli maelezo ya ufufuko yalikuwa uongo. Kitu gani waligundua?
Kuangalia ushuhuda wa madai makuu
yaliyowahi kufanyika ya ufufuko wa Yesu Kristo!
No comments:
Post a Comment