HISTORIA YA KALE HADI FREEMASONS
Mara nyingi nimekuwa nikijiuliza ni kwanini majina ya miungu wa kigiriki na wale wa Kirumi, ambao ustaarabu wao pia umechanulia mashariki ya kati ilikuwa ikiyatumia majina ya sayari kama majina ya miungu yao?
Walizijua vipi sayari hizo na majina yake enzi hizo za maelfu ya miaka kabla ya Masihi?. Nia yangu si kupatiwa majibu lakini kilicho kikubwa ni kwamba millennia nyingi wakati wa mpango mkubwa wa kuichukua dunia ili iwe ya kabila fulani moja tu;
Taarifa nyingi kuhusu historia ya kweli ya dunia zimekuwa zikifichwa na kupewa watu maalum kama ambavyo tutakavyoona huko mbele.

Kwa maelfu ya miaka dunia imekuwa ikipitia mabadiliko na misukosuko kadhaa lakini hakuna hata moja lililopata kuelezewa na wale wanaoitwa WANAHISTORIA kwasababu si kazi yao.
Kazi yao ni kufundisha kile tu walichoambiwa na kuelekezwa wakifundishe. Masalio mengi ya kihistoria, yaliyopatikana miaka ya hivi karibuni ngesaidia kuibadili historia inayotumika hivi sasa. Kinachoshangaza yamewekwa kama mapambo kwenye majumba ya makumbusho.

Kwa miaka mingi sasa mfumo wa elimu umekuwa wa kukitukuza kile kilochofanywa na wasomi waliotangulia, wala hautoi nfasi kwa wasomi wa sasa nao kuwa wabunifu na hivyo kuleta maarifa mapya.
KWANINI?
Mtu kunakili kilichoandikwa kitabuni anaonekana kuwa na akili sana na mtu anayeelewa vyema somo.; Yule nayejaribu kuelezea kwa maneno yake ili kuonyesha ubunifu wake wa namna alivyolielewa somo husika nje ya mstari na nukta za vitabuni anaonekana hajui kitu kwa hiyo amekosea.
Huo ndio mfumo uliotengeneza tangu enzi na enzi ili kufanya binadamu awe mjinga maisha yake yote ili hali mkononi anacho cheti kinachomtambulisha kuwa ana shahada moja, mbili, tatu hata nne. Lakini kichwani mwake ni kama maktaba iliyojaa vitabu vilivyoandikwa na wengine.

MBINU kubwa waliyoitumia ana ambayo bado inatiliwa msisitizo kwa njia mbalimbali ni kuwafanya watu wa makabila mengine waendelee kuwa WAJINGA na WAPUMBAVU wa mwisho kabisa. Elimu na yale maarifa ya ukweli, wakayachukua wao.
KWA LEO NIISHIE HAPA