Friday, September 28, 2012

HUYU NDIYE RAIS TUNA MUHITAJI DSJ
Usomi wa ngazi mbalimbali si sifa ya mtu kufaa kuwa kiongozi, dunia katika historia yake ina majina lukuki ya baadhi ya viongozi ambao walikuwa wasomi, lakini hatima ya uongozi wao haikutofautiana na wajinga.

Hata hapa nchini kuna baadhi ya viongozi serikalini, kwenye mashirika na hata kwenye sekta binafsi ambao wakikuonesha vyeti vyao vya shule unaweza kuogopa, lakini utendaji wao ni kichefuchefu.

Tukiwa tunaelekea katika uchaguzi mkuu wa viongozi wa serikali ya wanafunzi (DASJOSO), wanafunzi wa DSJ wanatakiwa kuangalia kiongozi ambaye ataweza kuisogeza mbali serikali ya wanafunzi (DASJOSO)  na mwenye uono wa mbali kwa maendeleo ya serikali na chuo kwa ujumla.

Kisaikolijia sifa za kiongozi ziko wazi na ni muhimu, mtu kuwa nazo kabla au baada ya kupewa cheo. Leo tunataka kuziangalia kwa undani sifa hizi, ili kama wanafunzi  wenye dhamana ya kuchagua watu wa kuongoza tuwatazame watu kwa sifa zao kabla na baada ya kuwapa nafasi. Sifa za kiongozi ni hizi zifuatazo:

Awaze mafanikio makubwa
Raisi wa Dasjoso lazima awe na maono ya juu ya kuhakikisha kuwa , serikali ya wanafunzi inapata mafanikio makubwa, hii ndiyo itakuwa dira ya kazi yake itakayompa muongozo wa kusimamia  watendaji wote walio chini yake kufikia kiwango cha mafanikio anachokiwaza. Kiongozi asiyekuwa na mawazo ya juu ya kuendelea kutoka mahali alipo hafai kuongoza.

Awe na nia
Haitoshi kwa Rais kuwa na mawazo chanya peke yake bila kuwa na nia ya kuyatimiza. Hivyo, Rais atafaa kuchaguliwa kuwa kiongozi endapo tu atakuwa na uwezo wa kuratibu vema na kutekeleza alichowaza. Ajue njia anayopita, awatangulie anaowaongoza kwa vitendo.

Ajitambue mwenyewe
Lazima kiongozi ajitambue mwenyewe ni mtu wa namna gani, ajue uwezo wake na upungufu wake na awe tayari kujiongezea maarifa kila siku, ili aweze kukabili changamoto na mabadiliko ya ulimwengu. Asome, afuatilie mambo yanavyokwenda na ajifunze kwa wenzake kuhusu kufanikisha malengo yake.

Asimamie maamuzi
Kuna wakati malengo hukumbana na vikwazo, hivyo ni wajibu wa Rais kusimamia maamuzi sahihi na kuwa mtu wa mwisho. Kiongozi mwenye kubadilika badilika kama kinyonga, hafai kwa vile kukosa msimamo kuna maanisha udhaifu wa mipango na kujiamini.

Adhibiti msongo wa mawazo
Tunamtarajia kiongozi mzuri awe ni mtu mwenye kupunguza msongo wa mawazo, ili kuifanya akili yake ifikie maamuzi sahihi, lakini kama atakuwa mwenye kuwaza mengi, atajikuta anachanganyikiwa na kuwa mtu wa jazba katika maamuzi na hivyo kuipotosha jamii.

Akubali kukosolewa
Viongozi wasiokuwa na sifa za uongozi huwa hawakubali kukosolewa, wakidhani kuwa hiyo ndiyo njia ya kuthibitisha msimamo wao na usahihi wao. Kiongozi makini ni yule ambaye atakuwa tayari kukosolewa na kuwapongeza wanaomkosoa kwa kutazama mwenendo wake na usahihi wake. Asiyekubali kukosolewa hafai kuwa kiongozi.

Awe msikilizaji
Rais mzuri ni yule ambaye atakuwa tayari kuwasilikiza watu walio chini yake, apokee maoni yao na ikiwezekana ayafanyie kazi. Lakini pia anatakiwa kuwafahamu kwa undani, ili aweze kuwaongoza vema kufuatana na hali zao. Akiwa na watu walemavu wenye kasoro kadhaa wa kadhaa anatakiwa kuwatambua kabla na baada ya kuwa kiongozi wao. Kuongoza usichokifahamu ni ujinga.

Afuate haki
Kiongozi imara anatakiwa kufuata haki katika kuongoza kwake, asijione mwenye haki zaidi ya wale anaowaongoza katika sheria. Ni muhimu kwake kuwafanya walio chini yake kujiona wako huru katika mawazo na matendo. Kiongozi anayetumia nguvu na ukali kuongoza watu hafai. Hata yule mwenye kujivunia uongozi wake naye hafai.

Awe egemeo la watu
Sifa nyingine ya rais ajaye awe egemeo la watu wake katika shida na raha. Kiongozi mzuri ni yule ambaye atakuwa tayari kusikitika, kuomboleza, kufurahi pamoja na watu wa chini yake bila kujitenga nao. Ajitolee kuwatumikia watu kwa hali na mali na awe tayari kutumika zaidi kwa maslahi ya wengine.

Atie moyo watu

Raisi wa DASJOSO ajaye anatakiwa kuwa na uwezo wa kuwatia moyo walio chini yake ili waweze kuendeleza vipaji vyao. Haipendezi kwa kiongozi kuwavunja moyo watu kwa kauli za kudharau kazi na jitihada zao walizojaribu kufanya katika kutekeleza majukumu yao kama wafanyakazi au wananchi.

Afurahie mafanikio

Sifa nyingine muhimu ya Rais tunaye mtaka awe tayari kufurahia mafanikio aliyopata pamoja na watu wake. Ni wajibu wa kiongozi kutoa tuzo, kuwashukuru wafanyakazi wake na kuwa tayari kuwapa ofa. Hii itasaidia kuwafanya watu waone hawajapoteza nguvu zao katika utendaji wao na kwamba wanakubalika. Si busara wakati mwingine kuwakosoa watu mbele ya hadhara na kueleza kutofurahishwa na kazi zao.

Aungane na wa chini yake

Mtu kuwa Rais haimaanishi amekuwa wa tofauti na watu wengine kiasi cha kushindwa kuchangamana nao kama wanavyofanya baadhi ya viongozi. Rais mwema ni yule atakayeungana na watu wake katika maisha ya kawaida. Kuwa kiongozi haimaanishi kwamba watu watakufuata wewe kila siku, wakati mwingine wewe unatakiwa kuwafuata wao na kuwa nyuma yao hata mahali walipokosea au wanapokabiliwa na makosa, watetee na uoneshe kuwajali na kuwapigania, makosa utayahesabu baada ya utetezi wako kukamilika.

Akubali lawama
Kama Rais akifanya mambo ambayo jamii haikupendezwa nayo anachotakiwa kufanya ni kukubali kulaumiwa. Ikiwa anaongoza kitego cha umeme kwa mfano na watu hawakupata nishati hiyo kwa wakati hatakiwi kukwepa lawama, vivyo hivyo kwenye wizara na idara au nchi kwa ujumla.

Afahamu kutatua matatizo
Raisi tunaye mwitaji ni yule ambaye atakuwa na uwezo wa kuzuia migogoro na kuitatua kwa haraka. Muongozo mzuri katika eneo hili umesimama katika mawasiliano na watu wa chini, mawasiliano haya ndiyo yatakayomuwezesha kiongozi kujua matatizo waliyonayo wafanyakazi wake au hata jamii anayoiongoza na hivyo kumfanya apate wasaa wa kuyashughulikia mapema.

Ajifunze kwa makosa
Wakati mwingine mawazo na mipango inaweza ikaenda kombo, hivyo ni wajibu wa Rais atatakiwa kujifunza kutokana na makosa yake au ya wale anaowaongoza, ili kuepuka kurudia makosa yale yale na kumfanya apoteze sifa za kuwa kiongozi mzuri.
Mwanafalsafa Winston Churchill aliwahi kusema "The price of greatness is responsibility." Thamani ya ukuu ni uwajibikaji.

Awe mwaminifu
Miongoni mwa maeneo magumu kabisa yaliyowashinda na yanayoendelea kuwashinda viongozi wengi ni uaminifu. Rais wa DASJOSO anatakiwa awe tayari kusimamia muongozo wa katiba ya nchi au marufuku alizowekewa katika madaraka yake. Hii inakwenda sambamba na kutowaonea, kuwanyanyasa wa nchini yake kwa kutumia cheo chake.

Awe mkweli
Viongozi wengi hasa wa kisiasa siku hizi ni waongo hakuna mfano, wamejaa ahadi zisizotekelezeka na hata wanapogundua kuwa hawana uwezo au wamekwama kuzitimiza, hawaoni haja ya kutubu mbele ya wanaowaongoza. Kiongozi makini ni yule atayekuwa tayari kuonesha ubora wa matendo na kauli zake.

Asiwe mwenye majungu
Kuna baadhi ya viongozi kwenye maofisi wanaendekeza sana majungu na pengine kuyapa umuhimu wa hali ya juu. Hii ni sifa mbaya kwa kiongozi yo yote, hivyo anayetumikia ‘umbea’ katika ofisi aliyokabidhiwa kama mkuu anapaswa kuondolewa. Kiongozi makini atatumia uwezo wake kuzuia watu wasimsengenye/wasisengenyane kwa kuwa muwazi na mwenye kufungua milango ya watu kumuona na kumlaumu na kueleza hisia zao.

Awe bora
Kwa kila analofanya kama rais lazima alifanye kwa ubora, asiwe mtu mwenye kulipua kazi na kufanya chini ya kiwango cha uwezo wake. Kila siku katika kazi, maamuzi, usimamizi, utekelezaji lazima atumike zaidi ya uwezo wake.

Nguzo imara ya mwanafunzi yeyote anayetaka kufanikiwa katika masomo yake ni kuwa mfuasi wa UTII na UAMINIFU mahali popote na kwa mtu yeyote. Nakumbuka wakati nikiwa shule ya sekondari nilikiuka sana mambo haya muhimu, nilikuwa mtu wa vurugu na mwanzilishi wa migomo.

MBINU  ZA KUMTAMBUA MWANAMKE ANAYEKARIBIA KUMUACHA MWANAUME

Kuna tofauti kubwa ya kimaamuzi kati ya mwanaume na mwanamke kwenye suala la kuachana. Inaelezwa kwamba, wanaume ni rahisi kwao kuamua ndani ya dakika moja na kutangaza kuvunja uhusiano, lakini kwa wanawake maamuzi yao mara nyingi hutanguliwa na dalili, ingawa hata wanaume nao wanazo.

Uchunguzi unaonesha kuwa, wanawake wengi hawawezi kuficha sana hisia zao za mapenzi, lakini pia kwenye chuki hawakujaaliwa uvumilivu. Wanasaikolojia wanakiri kwamba, kutambua mawazo yaliyomo ndani ya mwanamke kwa kumtazama muonekano wake usoni ni rahisi kuliko mwanaume ambaye anatajwa kuwa na uwezo kuficha mawazo yake.

Muongozo huo wa kitaalamu wa kumtambua mwanamke anayekaribia kukuacha ni kazi rahisi, ambayo inaweza kuanzia kwenye kona ya mazoea ya tabia zake za kila siku kwenye uhusiano wa kimapenzi. Ni imani yangu kuwa kila mwanaume anamfahamu mpenzi wake katika sura mbili za chuki na furaha yake.

Atakuwa mwanaume wa ajabu ambaye atarudi nyumbani kwake na kushindwa kusoma sura ya mkewe na kujua kama ana furaha au amekwazika.
Ninapotazama uwezekano rahisi wa kumtambua mwanamke, nafika mahali pa kuamini kuwa dokezo chache nitakazotoa hapa chini zinaweza kuwa msaada kwa wanaume wengi kujua kama wamekaribia kuwekwa kando kimapenzi.

KUPENDA KUJITENGA
Mwanamke ambaye anapenda kujitenga na mpenzi wake atakuwa kwenye hatua za awali za kuelekea kuachana naye. Tabia ya mwanamke kutopenda kukaa karibu na mumewe au mpenzi wake inatajwa kama ishara ya kuchoka au kukinai penzi. Hoja inabaki pale niliposema pa yeye kushindwa kuamua haraka na hivyo kutengeneza kwanza hali ya kumpuuza mpenzi wake.

KUPOTEZA HAMU YA TENDO LA NDOA
Mwanamke ambaye hafurahii tendo la ndoa kwa mumewe au mpenzi wake yuko kwenye hatua za kuacha. Mara zote msisimko wa kimapenzi huashiria utoshelevu wa kihisia ambao ndiyo unaoelezwa kuwa ni muhimu kwenye uhusiano wa kimapenzi kuliko kitu kingine chochote.
Hii ina maana kwamba, mwanamke anayetosheka na kuvutiwa na mwanaume aliyenaye hawezi kukosa hisia za kimapenzi hasa anapokuwa na mwenza wake faragha.

KUPENDA KUKOSOA
Kama nilivyosema, kujua historia ya penzi lenu namna lilivyoanza ni jambo muhimu kwa sababu husaidia kujua kama kuna mabadiliko hatari ya tabia za mwanamke.
Ikitokea mpenzi wako ambaye hapo mwanzo alikuwa msikivu na ghafla ukaanza kuona amekuwa mkosaji na mpingaji wa mwenendo wako au kila unachofikiria kukifanya, tambua kuwa hiyo ni ishara kuwa amechoka kilichobaki ni nafasi ya kukuacha.

UHUSIANO NA MTU MWINGINE
Licha ya kwamba usaliti kwenye uhusiano limekuwa suala la kawaida siku hizi, lakini mwanamke ambaye atakuwa hafichi uhusiano wake wa pembeni na kuacha minong’ono ikikufikia huku yeye akionesha kutojali malalamiko yako ya kusalitiwa, ujue hiyo ni ishara kwamba mwanaume wa pembeni amemfikisha kwenye hitaji la moyo wake na hivyo kuachana na wewe si jambo la gharama kwake. 

KUTOKUKUTEGEMEA
Mwanamke ambaye ana kusudio la kukuacha huanza kwa kuuondoa utegemezi. Ikiwa alikuwa anakuomba nauli, fedha ya matumizi, ada na huduma nyingine atasitisha bila kukuambia na bado utaona anaendelea kujimudu kama kawaida au kuteseka kimya kimya. Kuacha kukutegemea kama zamani ni dalili za kuweza kuishi bila wewe na hivyo kutafsiri

Posted by manyotablogspot.com, May 8, 2011 1 comments

Kwenye mapenzi kuna nyakati za kutofautiana, kukasirishana. Katika hali ya kawada kipindi hiki huwa ni za hatari kwa sababu husababisha nyufa kubwa za uhusiano na kulifanya penzi kukosa ladha.
Sote tunajua, watu hupigana, huachana, hujeruhiana, hutukanana, hudhalilishana wakiwa na hasira. Hata hivyo si wote wanaojua wafanye nini wanapojikuta wameingia kwenye hatua hiyo mbaya.

Msomaji wangu, hebu jaribu kukumbuka ugomvi mmoja uliotokea kati yako na mpenzi wako na ikiwezekana jikumbushe mlivyoanza! Utabaini kuwa mlianza kama utani na mkajikuta mmefura kwa hasira, mkatwangana makonde, mkatamkiana maneno makali ya kuudhi na pengine mkaamua kuachana.

Yote hii ni kwa sababu mlikosa elimu ya mazungumzo. Ingekuwa mmoja wenu hasa yule aliyekuwa wa pili kukasirika anafahamu hatua za kuzungumza na mtu aliyekasirika angechukua jukumu la kutuliza machafuko na kuleta amani kwenye mapenzi. Tazama hatua tano za kuzungumza na mpenzi aliyekasirika.

MPUNGUZE MHEMKO
Hasira hujaza kifua, huathiri mzunguko wa damu na ufahamu. Mtu aliyekasirika huwa vigumu kwake kusikiliza au kutazama mambo kwa jicho la tatu. Mwenye hasira huwa hafikirii matokea yajayo badala yake hutazama zaidi tukio na jinsi ya kupata ushindi iwe kwa maneno au kwa mapambano.

Katika hali ya namna hiyo, mtu mwingine akija na busara za kutaka kumgeuza haraka haraka hawezi kumuelewa. Muhimu hapo ni kuacha kumwadama, kujibizana naye, kumshawishi asikilize badala yake mpe nafasi ya kusema atakavyo, abwate ajuavyo huku wewe ukimuitikia na kumkubalia lawama zake. “Basi mpenzi mwenye makosa ni mimi.” Kauli za aina hii zitampunguza hasira kwani atajiona msindi.

MSOME SAIKOLOJIA YAKE
Kwa kuwa unamfahamu mpenzi wako kwa kina itakuwa rahisi kwako kumtambua kuwa amepunguza hasira na kurudi katika hali yake ya kawaida. Ukisha fahamu hilo chukua jukumu la kumsoma kisaikojia ili kujua kama yuko kwenye hali nzuri ya kusikiliza yale uliyotaka kumwambia wakati alipokuwa na hasira.

Zoezi hili linaweza kuchukua saa kadhaa na wakati mwingine hata siku mbili. Lengo ni nini? Ni kupata matokeo sahihi ya kuondoa chuki za mwenza wako na kumfundisha madhara ya kukasirika kwenye uhusiano wenu wa kimapenzi. “J, nakupenda sana, lakini juzi uliniumiza, uliniambia mimi malaya kwa kosa ambalo sikufanya?” Bila shaka muda huo atakusikiliza zaidi kuliko ungebishana naye alipokuwa na hasira.

MRUHUSU AKUJIBU
Pamoja na kumsoma kisaikojia na kumwambia kinagaubaga makosa yake, usimzuie kujitetea, mpe nafasi ya kuzungumzia kilichomkasirisha. “Unaona bado unanitukana, sasa naamini siku ile ulikuwa umedhamilia.” Usisiseme hivyo, mwache ajibu hoja hata kama atakuwa anakukandamiza na kuzidi kujijengea ushindi. Mvumilie aoshe ubongo wake.

EPUKA MARUMBANO
Kama nilivyosema kwenye hapo juu, wapenzi wengine huwa wagumu kuelewa, ni watu wa kuficha udhaifu wao na kutopenda kuonekana wamekosea. Watu wa namna hii unapowarejeshea mazungumzo wanaweza kujikuta wanahamaki tena.
“Kwa hiyo ulikuwa unasemaje…nilifanya ndiyo,… wewe unaamuaje?” Mkifika kwenye alama hiyo usikubali kurumabana naye mwache aseme halafu wewe ingia kwenye hatua ya tano.

MUOMBE MSAMAHA
Hata kama atakuwa yeye ndiye mwenye makosa na amekataa kukiri, usijali, chukua jukumu la kumuomba msamaha na kueleza tena nia yako ya kumazungumzo ilikuwa ni kuelewana si kugombana. Kumbuka hata kama amekiri kosa, bado unatakiwa kumuomba radhi kwa kurejea yaliyopita. “Mpenzi inawezekana nikawa nimekuudhi kwa niliyosema, nakuomba sana tusameheane.”

Bila shaka kwa haya machache msomaji wangu utakuwa umejifunza na kuchukua hatua za kuzuia migogoro mikubwa inayotokana na hasira za mpenzi wako. Leo niishie hapa, nikushukuu kwa kunisoma

Jinsi ya kuzungumza na mpenzi wako aliyekasirika Posted by manyotablogspot.c

om, May 8, 2011 1 comments