Waandishi wakubali kubadilika, wajifunze Kiswahili
wasirudie makosa
|
|
|
Na Cosmas Pahalah
KATIKA makala yafuatayo nimetoa maelezo ambayo yana lengo la kusisitiza baadhi ya mambo yaliyoelezwa hapo awali. Lengo ni kuimarisha uelewa wa misingi ya lugha sanifu ya Kiswahili. Kwa mfano: “ Misitu ya Kazimzimbwi na Pugu iko katika hatari ya kuvamiwa na wananchi kwa ajili ya kuvuna miti ya kuchomea mkaa.” Katika sentensi hii msomaji ataelewa kuwa iko miti ya kuchomea mkaa kwa maana ya kuwa miti ni kichocheo cha kuchoma mkaa. Ukweli ni kuwa miti inachomwa na matokeo yake ni upatikanaji wa mkaa. Kwa hiyo, sahihi ni kuandika, “…kwa ajili ya kuvuna miti ya kuchoma mkaa.” “Kwa bahati nzuri, nilipata fursa ya kuhudhuria mikutano ya kampeni na moja ya mikutano niliyohudhuria ndiyo msingi wa makala hii.” Ni kawaida kwa maneno yanayoanza na ‘ma’ kama vile mahitaji, madhumuni, maradhi na kadhalika, neno linalofuata Tunasema makala haya na wala siyo makala hii. Nafahamu kuwa watu wengi wamezoea kuandika makala hii, lakini mazoea yasiwe kisingizio cha kuendeleza makosa. Ni vigumu kubadilika baada ya kuzoea aina fulani ya mazoea, hivyo hatuna budi kubadilika. “ Lugha zilizokuwa zikitumiwa na baadhi Wakati mwandishi alipoandika taarifa hii alisema kuwa wazungumzaji walitumia lugha za kejeli. Ukweli ni kuwa lugha iliyotumika ni ya Kiswahili na wala siyo zaidi. Katika lugha hii, wazungumzaji walitumia maneno ya matamshi ya kejeli na matusi ambayo yalikuwa ni ya udhalilishaji. Hivyo, ingekuwa bora “ Kitu kilichomfanya awe na wakati mgumu ni kwa mpira ilikuwa wa kasi na wenye rafu nyingi.” Hapa siyo kitu kimoja kichomfanya awe na wakati mgumu bali ni mambo mengi yakiwamo kasi ya mpira na pia rafu nyingi. Liko neno lililotumika la ‘ilikuwa’ lililotumika kimakosa. Ilitakiwa liwe ‘kuwa’. Kwa hiyo, angeandika, “Kitu kilichomfanya awe na wakati ngumu ni kwa mpira kuwa wa kasi na wenye rafu.” “ Hoteli ya Kwa bahati mbaya mwandishi ana taaluma ndogo ya sarufi kwani ameshindwa kutambua matumizi sahihi ya ‘o’ rejeshi. Badala ya kuandika ‘masanduku ya kura yaliingia katika ngome ya CCM’ alitakiwa kuandika masanduku ya kura yaliyoingia katika ngome ya CCM. “Kwa mfano, ukichukua takwimu za wanafunzi kutoka wilayani ukilinganisha na zilizoko mikoani utakuta zinakataana.” Neno linaloleta mushkeli hapa ni ‘kukataana’. Maana ya kukataa ni kusema au kuonyesha kwa vitendo kutokubali jambo fulani , kusema hapana, kuzuia au kunyima. Sasa tunaposema kuwa takwimu zimekataana tuna maana ya kunyima, kuzuia au kusema hapana. Maneno yote hayo hayaelekei kukaribia maana iliyokusudiwa. Neno ambalo lingefaa hapa ni kutofautiana. Kwa maana hiyo, takwimu zilitofautiana kati ya zile za wilayani na zile za mikoani. Upo mtindo wa waandishi wa magazeti kuendelea kutumia neno maamuzi badala ya uamuzi. Angalia sentensi zifuatazo ambazo zimetokana na waandishi wawili tofauti na katika nyakati tofauti: “Haya ndiyo maamuzi magumu ya Pep Guardiala.” “Hakika hakuna njia nyingine iwapo Jaji huyo, alitoa siri iliyoko kwenye maamuzi kwa mtu mwingine wa pili”. Kwa kuzingatia uandishi bora, maneno “Askofu Telesphory Mkude alisema hakuna budi kwa Watanzania kuishi katika maisha ya upendo na amani Matumizi ya ‘budi’ yanawakanganya watu wengi. Yafaa ieleweke kuwa tunapotumia neno budi tuna maana ya hiyari lakini tunapolitumia hatuna budi, hapana budi, sina budi, hawana budi tuna maana ya kusema ni lazima. Kwa hiyo, ni muhimu kufahamu kuwa ukisema ni budi niende maana yake una hiyari ya kwenda. “Mungu amekuwa akimsamehe kila mtu dhambi zake hususani wale wanaotambua na kumrejea kumwomba awasamehe.” Kwa kawaida, maneno ya Kiswahili na hata yale yanayotoholewa, yanafuata msingi wa lugha ya Kiswahili usemao kuwa ni lazima kuishia na irabu (a, e, i, o, u). Hata hivyo, tunayo maneno machache ambayo hayafuati kanuni hii. Maneno haya ni “Kamati yake inasisitiza kuwa halmashauri zote za Mkoa wa Lindi kutunga sheria ndogo mpya kwa kutambua dhumuni la sheria hizo.” Katika kipindi kilichopita niwahi kueleza kuwa yako maneno ambayo hayana wingi bali yana umoja tu ijapokuwa neno lenyewe limeanza na kiambishi ma-. Kwa mfano yako maneno Katika Kiswahili hatuna maneno Kwa upande mwingine, tunayo maneno |
MAPISHI
‘FISH FINGER’
Karibu sana katika safu hii ya mapishi ambapo leo
ninakuletea upishi wa chakula kinachoitwa ‘ Fish Finger’. Ungana nami
mtayarishaji wako Cosmas Pahala.
1.
Samaki wakubwa
kiasi
2.
Nyanya 5
3.
Hoho 1
4.
Karoti 1
5.
Nyanya kopo 1
6.
Chumvi kiasi
7.
Vitinguu maji na
saumu
8.
Mafuta ya kupikia
9.
Pilipili 3
10.
Ndimu
Jinsi ya kupika
1.
Kausha vipande
vitatu vitatu kwa jua, vikisha kauka visage kwa kutumia blenda (kifaa maalum
cha kusagia), vikiwa tayari weak kwenye sahani.
2. Paka samaki
wako chumvi, twanga vitunguu saumu uweke samaki, tia ndimu na maji
kiasi.kwenye
3. Bandika jikoni acha yachemke mpaka maji yote
yachemke. Toa miiba ya samaki.
4.
Changanya samaki
wako mpaka wachanganyike kabisa kasha viringisha vipande vipande kama vidole.
5.
Weka kwenye ule
unga wa mkate ulio kwisha usaga, vunja mayai na tumbukiza vipande kwenye mayai.
6.
Weka mafuta
jikoni yapate moto tumbukiza ‘fish finger’ zako ambazo ulizipaka unga wa mkate
na mayai.
7.
Acha mpaka ziwe
na rangi ya kahawia na uzitoe na kuziweka kwenye chombo kisafi, na hapo
zitakuwa tayari kwa kuliwa.
SHAIRI
MISAADA
YA WAGENI
Wazungu
wanayo nongwa, Haki wanatudhulumu
Wanaleta
ya paukwa, Twabaki mashamusham
Kila
tunacholetewa, Mwishowe twajilaumu
Misaada
ya wazungu, Ona inavyo tutesa.
Serikali
kuelewa, Hii inawalazimu
Misaada
mnayopewa, Ndani ndani yake kunabomu
Tusipende
vya kupewa, Tukumbuke ya mwalimu
Misaada
ya wazungu, Ona inavyotutesa.
Kanisa
tumeambiwa, Hii ni ya kwetu zamu
Mitumba
tunaletewa, Na fedha za kujikimu
Majengo
tunajengewa, Ila hili tuheshimu
Misaada
ya wazungu, Ona inavyo tutesa.
Ndoa
ya jinsia sawa, Zifungishwe kwa hakimu
Ndoa
ya jinsia sawa, Ati yaitwa karamu
Mwanaume
sawasawa, Kuolewa si haramu?
Misaada
ya wazungu, Ona inavyo tutesa.
Mashehe
wetu wazawa, Nawachungaji hudumu
Hii
ni chemsha kinywa , Sasa ni yakwetuzamu
Wazee
kwetu ni dawa, Tunusuruni kaumu
Misaada
ya wazungu, Ona inavyo tutesa
HUYU NDIYE RAIS TUNAYE MUHITAJI DSJ
Usomi wa ngazi mbalimbali si sifa ya mtu kufaa kuwa kiongozi, dunia katika historia yake ina majina lukuki ya baadhi ya viongozi ambao walikuwa wasomi, lakini hatima ya uongozi wao haikutofautiana na wajinga.
Hata hapa nchini kuna baadhi ya viongozi serikalini, kwenye mashirika na hata kwenye sekta binafsi ambao wakikuonesha vyeti vyao vya shule unaweza kuogopa, lakini utendaji wao ni kichefuchefu.
Tukiwa tunaelekea katika uchaguzi mkuu wa viongozi wa serikali ya wanafunzi (DASJOSO), wanafunzi wa DSJ wanatakiwa kuangalia kiongozi ambaye ataweza kuisogeza mbali serikali ya wanafunzi (DASJOSO) na mwenye uono wa mbali kwa maendeleo ya serikali na chuo kwa ujumla.
Kisaikolijia sifa za kiongozi ziko wazi na ni muhimu, mtu kuwa nazo kabla au baada ya kupewa cheo. Leo tunataka kuziangalia kwa undani sifa hizi, ili
Awaze mafanikio makubwa
Raisi wa Dasjoso lazima awe na maono ya juu ya kuhakikisha kuwa , serikali ya wanafunzi inapata mafanikio makubwa, hii ndiyo itakuwa dira ya kazi yake itakayompa muongozo wa kusimamia watendaji wote walio chini yake kufikia kiwango cha mafanikio anachokiwaza. Kiongozi asiyekuwa na mawazo ya juu ya kuendelea kutoka mahali alipo hafai kuongoza.
Awe na nia
Haitoshi kwa Rais kuwa na mawazo chanya peke yake bila kuwa na nia ya kuyatimiza. Hivyo, Rais atafaa kuchaguliwa kuwa kiongozi endapo tu atakuwa na uwezo wa kuratibu vema na kutekeleza alichowaza. Ajue njia anayopita, awatangulie anaowaongoza kwa vitendo.
Ajitambue mwenyewe
Lazima kiongozi ajitambue mwenyewe ni mtu wa namna gani, ajue uwezo wake na upungufu wake na awe tayari kujiongezea maarifa kila siku, ili aweze kukabili changamoto na mabadiliko ya ulimwengu. Asome, afuatilie mambo yanavyokwenda na ajifunze kwa wenzake kuhusu kufanikisha malengo yake.
Asimamie maamuzi
Kuna wakati malengo hukumbana na vikwazo, hivyo ni wajibu wa Rais kusimamia maamuzi sahihi na kuwa mtu wa mwisho. Kiongozi mwenye kubadilika badilika
Adhibiti msongo wa mawazo
Tunamtarajia kiongozi mzuri awe ni mtu mwenye kupunguza msongo wa mawazo, ili kuifanya akili yake ifikie maamuzi sahihi, lakini
Akubali kukosolewa
Viongozi wasiokuwa na sifa za uongozi huwa hawakubali kukosolewa, wakidhani kuwa hiyo ndiyo njia ya kuthibitisha msimamo wao na usahihi wao. Kiongozi makini ni yule ambaye atakuwa tayari kukosolewa na kuwapongeza wanaomkosoa kwa kutazama mwenendo wake na usahihi wake. Asiyekubali kukosolewa hafai kuwa kiongozi.
Awe msikilizaji
Rais mzuri ni yule ambaye atakuwa tayari kuwasilikiza watu walio chini yake, apokee maoni
Afuate haki
Kiongozi imara anatakiwa kufuata haki katika kuongoza kwake, asijione mwenye haki zaidi ya wale anaowaongoza katika sheria. Ni muhimu kwake kuwafanya walio chini yake kujiona wako huru katika mawazo na matendo. Kiongozi anayetumia nguvu na ukali kuongoza watu hafai. Hata yule mwenye kujivunia uongozi wake naye hafai.
Awe egemeo la watu
Sifa nyingine ya rais ajaye awe egemeo la watu wake katika shida na raha. Kiongozi mzuri ni yule ambaye atakuwa tayari kusikitika, kuomboleza, kufurahi pamoja na watu wa chini yake bila kujitenga nao. Ajitolee kuwatumikia watu kwa hali na
Atie moyo watu
Raisi wa DASJOSO ajaye anatakiwa kuwa na uwezo wa kuwatia moyo walio chini yake ili waweze kuendeleza vipaji vyao. Haipendezi kwa kiongozi kuwavunja moyo watu kwa kauli za kudharau kazi na jitihada zao walizojaribu kufanya katika kutekeleza majukumu
Afurahie mafanikio
Sifa nyingine muhimu ya Rais tunaye mtaka awe tayari kufurahia mafanikio aliyopata pamoja na watu wake. Ni wajibu wa kiongozi kutoa tuzo, kuwashukuru wafanyakazi wake na kuwa tayari kuwapa ofa. Hii itasaidia kuwafanya watu waone hawajapoteza nguvu zao katika utendaji wao na kwamba wanakubalika. Si busara wakati mwingine kuwakosoa watu mbele ya hadhara na kueleza kutofurahishwa na kazi zao.
Aungane na wa chini yake
Mtu kuwa Rais haimaanishi amekuwa wa tofauti na watu wengine kiasi cha kushindwa kuchangamana nao
Akubali lawama
Kama Rais akifanya mambo ambayo jamii haikupendezwa nayo anachotakiwa kufanya ni kukubali kulaumiwa. Ikiwa anaongoza kitego cha umeme kwa mfano na watu hawakupata nishati hiyo kwa wakati hatakiwi kukwepa lawama, vivyo hivyo kwenye wizara na idara au nchi kwa ujumla.
Afahamu kutatua matatizo
Raisi tunaye mwitaji ni yule ambaye atakuwa na uwezo wa kuzuia migogoro na kuitatua kwa haraka. Muongozo mzuri katika eneo hili umesimama katika mawasiliano na watu wa chini, mawasiliano haya ndiyo yatakayomuwezesha kiongozi kujua matatizo waliyonayo wafanyakazi wake au hata jamii anayoiongoza na hivyo kumfanya apate wasaa wa kuyashughulikia mapema.
Ajifunze kwa makosa
Wakati mwingine mawazo na mipango inaweza ikaenda kombo, hivyo ni wajibu wa Rais atatakiwa kujifunza kutokana na makosa yake au ya wale anaowaongoza, ili kuepuka kurudia makosa yale yale na kumfanya apoteze sifa za kuwa kiongozi mzuri.
Mwanafalsafa Winston Churchill aliwahi kusema "The price of greatness is responsibility." Thamani ya ukuu ni uwajibikaji.
Awe mwaminifu
Miongoni mwa maeneo magumu kabisa yaliyowashinda na yanayoendelea kuwashinda viongozi wengi ni uaminifu. Rais wa DASJOSO anatakiwa awe tayari kusimamia muongozo wa katiba ya nchi au marufuku alizowekewa katika madaraka yake. Hii inakwenda sambamba na kutowaonea, kuwanyanyasa wa nchini yake kwa kutumia cheo chake.
Awe mkweli
Viongozi wengi hasa wa kisiasa siku hizi ni waongo hakuna mfano, wamejaa ahadi zisizotekelezeka na hata wanapogundua kuwa hawana uwezo au wamekwama kuzitimiza, hawaoni haja ya kutubu mbele ya wanaowaongoza. Kiongozi makini ni yule atayekuwa tayari kuonesha ubora wa matendo na kauli zake.
Asiwe mwenye majungu
Kuna baadhi ya viongozi kwenye maofisi wanaendekeza
Awe bora
Kwa kila analofanya
Nguzo imara ya mwanafunzi yeyote anayetaka kufanikiwa katika masomo yake ni kuwa mfuasi wa UTII na UAMINIFU mahali popote na kwa mtu yeyote. Nakumbuka wakati nikiwa shule ya sekondari nilikiuka
DALILI KUMI NA TATU ZA MIMBA
Na
Cosmas Pahalah
MWANAMKE anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za kawaida. Na ni wakati huo ambao ni muafaka kwake kuanza kuuchunguza mwili wake.
“Homoni zinazosambaa mwilini mara tu unapopata ujauzito husababisha mabadiliko kadhaa katika mwili wake ambayo yanaweza kugundulika kabla hata ya uchunguzi halisi wa kujua kama mjauzito au la,” anasema Melissa Goist, Profesa na Mtalaama wa Masuala ya Uzazi wa Chuo Kikuu chaOhio , Marekani.
Maumivu kwenye matiti
Hii ni dalili ya kawaida ya ujauzito ambapo nguvu za homoni mwilini huongezeka wakati yai linavyopata “rutuba”, jambo ambalo huongeza wingi wa damu na kuyafanya matiti ya mwanamke kuvimba na kuwa makubwa isivyo kawaida.
Maumivu mwilini
Utaanza kusikia maumivukama vile unataka
kuingia katika siku zako. Kwa kawaida hali hii hutokea wakati yai likiwa
linasafiri kwenda katika chumba cha mimba. Hivyo, hali hiyo husababisha sehemu
hiyo itanuke taratibu na kusababisha maumivu hayo.
Kutokwa damu bila kutegemea
"Wanawake wengi hufikiria kutokwa na damu kidogo ni dalili ya kuwa katika siku zao. Lakini, katika hali halisi, kutokwa damu kusikotegemewa, huwakumba asilimia 25 ya wanawake wakati wa kurutubika kwa yai,” anasema Goist. Ambaye anaendelea kusema kwamba iwapo utaona hedhi yako inakuwa fupi au inafanyika katika hali ambayo si ya kawaida, unashauriwa kwenda kufanya kipimo cha ujauzito..
Kuchoka
Unapojisikia kuchoka na kukosa raha, au kutaka hata kulala wakati ukiwa kazini, lazima ufahamu kwamba mwili wako unajirekebisha kuingia katika kipindi kipya cha mabadiliko.
“Tambua kwamba katika kipindi cha mwanzo cha ujauzito ni muda ambao mtoto tumboni huanza kutumia sehemu ya nguvu zako na hivyo kukuletea uchovu na usingizi” anasema Goist.
Chuchu kuwa nyeusi
Chuchu huanza kubadilika rangi yake kutokana na chembechembe za uhai (seli) kuanza kufanya kazi kwa nguvu zaidi. Hata hivyo, Goist anasema: “Wanawake wenye ngozi nyeusi hawawezi kuiona dalili hii mapema hadi muda wakama
wiki kumi zipite.”
Kichefuchefu
Hali hii huwapata asilimia 85 ya wanawake wanapopatwa na ujauzito, ambapo nyakati za asubuhi ndipo hasa hujionyesha.
Mwili kuvimba
Kuna wakati kupungua kwa nguvu za uyeyushaji chakula kunaweza kukusababishia kuona tumbo limevimba na nguo zikawa zinakubana kutokana na chakula kujaa katika utumbo. Lakini hali hiyo ikiendelea na ukaona siku zako haziji, basi ni vyema ukatambua kwamba tayari una ujauzito na kinachokupasa ni kwenda kuhakikisha.
Kwenda haja ndogo mara kwa mara
Kwenda haja ndogo kila mara ni dalili kwamba kibofu chako kimeanza kufanya kazi ya ziada, ambapo huwa kinafanya kazi ya kuondoa maji kwa uthabiti zaidi wakati wa ujauzito. Hali hii pia hujitokeza mwishoni mwa ujauzito, ambapo kibofu kitakapokuwa kinarudia hali yake ya kawaida baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu.
Tamaa ya vitu mbalimbali
Kutokana na mwili kuwa na “mzigo” wa ujauzito na hivyo kuchoka, hali hiyo humfanya mwanamke kutamani vitu mbalimbali ili kukidhi mabadiliko yaliyojitokeza katika mwili wake. Hii ni pamoja na kutaka vyakula fulani au kufanya mambo ambayo hapo nyuma alikuwa hayapendi.
Kuumwa kichwa
Kuongezeka kwa damu kunaweza kusababisha kichwa kuuma japokuwa sisana , hususani katika wiki
za mwanzo za ujauzito. Hata hivyo, hali hii hukoma mwili unapojirekebisha na
mzunguko wa homoni unaotokana na ujauzito.
Kufunga choo
Homoni ambazo husababisha mwili kuvimba pia husababisha kufunga choo kutokana na mfumo wa kuyeyusha chakula kutofanya kazi vyema. Hata hivyo hali hii inaweza kujitokeza zaidi wakati ujauzito unapoendelea kukua.
Kuwa na hasira
"Kutokana na kuongezeka kwa homoni za utendaji kazi mwilini, hali hiyo itakusababishia uchovu, na kukufanya kuwa na hasira,” anasema Goist
Kuongezeka kwa joto mwilini
Kipimo cha joto la mdomo ni muhimu katika kutambua hali ya ujauzito. Kwa kawaida joto huongezeka kwa nyuzi moja au zaidi wakati yai likiwa linatunga mimba. Hali hiyo ikiendelea kwa zaidi ya wiki mbili, itakuwa inaonyesha dhahiri kwamba kuna “mtoto anakuja”.
MWANAMKE anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za kawaida. Na ni wakati huo ambao ni muafaka kwake kuanza kuuchunguza mwili wake.
“Homoni zinazosambaa mwilini mara tu unapopata ujauzito husababisha mabadiliko kadhaa katika mwili wake ambayo yanaweza kugundulika kabla hata ya uchunguzi halisi wa kujua kama mjauzito au la,” anasema Melissa Goist, Profesa na Mtalaama wa Masuala ya Uzazi wa Chuo Kikuu cha
Maumivu kwenye matiti
Hii ni dalili ya kawaida ya ujauzito ambapo nguvu za homoni mwilini huongezeka wakati yai linavyopata “rutuba”, jambo ambalo huongeza wingi wa damu na kuyafanya matiti ya mwanamke kuvimba na kuwa makubwa isivyo kawaida.
Maumivu mwilini
Utaanza kusikia maumivu
Kutokwa damu bila kutegemea
"Wanawake wengi hufikiria kutokwa na damu kidogo ni dalili ya kuwa katika siku zao. Lakini, katika hali halisi, kutokwa damu kusikotegemewa, huwakumba asilimia 25 ya wanawake wakati wa kurutubika kwa yai,” anasema Goist. Ambaye anaendelea kusema kwamba iwapo utaona hedhi yako inakuwa fupi au inafanyika katika hali ambayo si ya kawaida, unashauriwa kwenda kufanya kipimo cha ujauzito..
Kuchoka
Unapojisikia kuchoka na kukosa raha, au kutaka hata kulala wakati ukiwa kazini, lazima ufahamu kwamba mwili wako unajirekebisha kuingia katika kipindi kipya cha mabadiliko.
“Tambua kwamba katika kipindi cha mwanzo cha ujauzito ni muda ambao mtoto tumboni huanza kutumia sehemu ya nguvu zako na hivyo kukuletea uchovu na usingizi” anasema Goist.
Chuchu kuwa nyeusi
Chuchu huanza kubadilika rangi yake kutokana na chembechembe za uhai (seli) kuanza kufanya kazi kwa nguvu zaidi. Hata hivyo, Goist anasema: “Wanawake wenye ngozi nyeusi hawawezi kuiona dalili hii mapema hadi muda wa
Kichefuchefu
Hali hii huwapata asilimia 85 ya wanawake wanapopatwa na ujauzito, ambapo nyakati za asubuhi ndipo hasa hujionyesha.
Mwili kuvimba
Kuna wakati kupungua kwa nguvu za uyeyushaji chakula kunaweza kukusababishia kuona tumbo limevimba na nguo zikawa zinakubana kutokana na chakula kujaa katika utumbo. Lakini hali hiyo ikiendelea na ukaona siku zako haziji, basi ni vyema ukatambua kwamba tayari una ujauzito na kinachokupasa ni kwenda kuhakikisha.
Kwenda haja ndogo mara kwa mara
Kwenda haja ndogo kila mara ni dalili kwamba kibofu chako kimeanza kufanya kazi ya ziada, ambapo huwa kinafanya kazi ya kuondoa maji kwa uthabiti zaidi wakati wa ujauzito. Hali hii pia hujitokeza mwishoni mwa ujauzito, ambapo kibofu kitakapokuwa kinarudia hali yake ya kawaida baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu.
Tamaa ya vitu mbalimbali
Kutokana na mwili kuwa na “mzigo” wa ujauzito na hivyo kuchoka, hali hiyo humfanya mwanamke kutamani vitu mbalimbali ili kukidhi mabadiliko yaliyojitokeza katika mwili wake. Hii ni pamoja na kutaka vyakula fulani au kufanya mambo ambayo hapo nyuma alikuwa hayapendi.
Kuumwa kichwa
Kuongezeka kwa damu kunaweza kusababisha kichwa kuuma japokuwa si
Kufunga choo
Homoni ambazo husababisha mwili kuvimba pia husababisha kufunga choo kutokana na mfumo wa kuyeyusha chakula kutofanya kazi vyema. Hata hivyo hali hii inaweza kujitokeza zaidi wakati ujauzito unapoendelea kukua.
Kuwa na hasira
"Kutokana na kuongezeka kwa homoni za utendaji kazi mwilini, hali hiyo itakusababishia uchovu, na kukufanya kuwa na hasira,” anasema Goist
Kuongezeka kwa joto mwilini
Kipimo cha joto la mdomo ni muhimu katika kutambua hali ya ujauzito. Kwa kawaida joto huongezeka kwa nyuzi moja au zaidi wakati yai likiwa linatunga mimba. Hali hiyo ikiendelea kwa zaidi ya wiki mbili, itakuwa inaonyesha dhahiri kwamba kuna “mtoto anakuja”.
No comments:
Post a Comment