Kuna tofauti kubwa ya kimaamuzi kati ya mwanaume na mwanamke kwenye suala la kuachana. Inaelezwa kwamba, wanaume ni rahisi kwao kuamua ndani ya dakika moja na kutangaza kuvunja uhusiano, lakini kwa wanawake maamuzi yao mara nyingi hutanguliwa na dalili, ingawa hata wanaume nao wanazo.
Uchunguzi unaonesha kuwa, wanawake
wengi hawawezi kuficha sana hisia zao za mapenzi, lakini pia kwenye chuki
hawakujaaliwa uvumilivu. Wanasaikolojia wanakiri kwamba, kutambua mawazo
yaliyomo ndani ya mwanamke kwa kumtazama muonekano wake usoni ni rahisi kuliko
mwanaume ambaye anatajwa kuwa na uwezo kuficha mawazo yake.
Muongozo huo wa kitaalamu wa kumtambua mwanamke anayekaribia kukuacha ni kazi rahisi, ambayo inaweza kuanzia kwenye kona ya mazoea ya tabia zake za kila siku kwenye uhusiano wa kimapenzi. Ni imani yangu kuwa kila mwanaume anamfahamu mpenzi wake katika sura mbili za chuki na furaha yake.
Atakuwa mwanaume wa ajabu ambaye atarudi nyumbani kwake na kushindwa kusoma sura ya mkewe na kujua kama ana furaha au amekwazika.
Ninapotazama uwezekano rahisi wa kumtambua mwanamke, nafika mahali pa kuamini kuwa dokezo chache nitakazotoa hapa chini zinaweza kuwa msaada kwa wanaume wengi kujua kama wamekaribia kuwekwa kando kimapenzi.
KUPENDA KUJITENGA
Mwanamke ambaye anapenda kujitenga na
mpenzi wake atakuwa kwenye hatua za awali za kuelekea kuachana naye. Tabia ya
mwanamke kutopenda kukaa karibu na mumewe au mpenzi wake inatajwa kama ishara
ya kuchoka au kukinai penzi. Hoja inabaki pale niliposema pa yeye kushindwa
kuamua haraka na hivyo kutengeneza kwanza hali ya kumpuuza mpenzi wake.
KUPOTEZA HAMU YA TENDO
LA NDOA
Mwanamke ambaye hafurahii tendo la ndoa kwa mumewe au mpenzi
wake yuko kwenye hatua za kuacha. Mara zote msisimko wa kimapenzi huashiria
utoshelevu wa kihisia ambao ndiyo unaoelezwa kuwa ni muhimu kwenye uhusiano wa
kimapenzi kuliko kitu kingine chochote.
Hii ina maana kwamba, mwanamke anayetosheka na kuvutiwa na mwanaume aliyenaye hawezi kukosa hisia za kimapenzi hasa anapokuwa na mwenza wake faragha.
Hii ina maana kwamba, mwanamke anayetosheka na kuvutiwa na mwanaume aliyenaye hawezi kukosa hisia za kimapenzi hasa anapokuwa na mwenza wake faragha.
KUPENDA KUKOSOA
Kama nilivyosema, kujua historia ya
penzi lenu namna lilivyoanza ni jambo muhimu kwa sababu husaidia kujua kama
kuna mabadiliko hatari ya tabia za mwanamke.
Ikitokea mpenzi wako ambaye hapo mwanzo alikuwa msikivu na ghafla ukaanza kuona amekuwa mkosaji na mpingaji wa mwenendo wako au kila unachofikiria kukifanya, tambua kuwa hiyo ni ishara kuwa amechoka kilichobaki ni nafasi ya kukuacha.
Ikitokea mpenzi wako ambaye hapo mwanzo alikuwa msikivu na ghafla ukaanza kuona amekuwa mkosaji na mpingaji wa mwenendo wako au kila unachofikiria kukifanya, tambua kuwa hiyo ni ishara kuwa amechoka kilichobaki ni nafasi ya kukuacha.
UHUSIANO NA MTU
MWINGINE
Licha ya kwamba usaliti kwenye
uhusiano limekuwa suala la kawaida siku hizi, lakini mwanamke ambaye atakuwa
hafichi uhusiano wake wa pembeni na kuacha minong’ono ikikufikia huku yeye
akionesha kutojali malalamiko yako ya kusalitiwa, ujue hiyo ni ishara kwamba
mwanaume wa pembeni amemfikisha kwenye hitaji la moyo wake na hivyo kuachana na
wewe si jambo la gharama kwake.
KUTOKUKUTEGEMEA
Mwanamke ambaye ana
kusudio la kukuacha huanza kwa kuuondoa utegemezi. Ikiwa alikuwa anakuomba
nauli, fedha ya matumizi, ada na huduma nyingine atasitisha bila kukuambia na
bado utaona anaendelea kujimudu kama kawaida au kuteseka kimya kimya. Kuacha
kukutegemea kama zamani ni dalili za kuweza kuishi bila wewe na hivyo kutafsiri
No comments:
Post a Comment